Ndege ndogo iliyowabeba abiria 21 imetoweka ikiwa maeneo yenye milima nchini Nepal.
Ndege
hiyo ilikuwa safarini kutoka Pokhara, magharibi mwa mji mkuu Kathmandu,
kwenda Jomsom, eneo ambalo watu wengi wanaoenda kukwea milima ya
Himalaya huanza safari yao ya kukwea milima hiyo.Hakuna viwanja vya ndege kati ya maeneo hayo mawili na inahofiwa kwamba ndege hiyo imeanguka.
Ndege hiyo ni ya shirika la ndege la Tara Airlines.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment