Klabu ya soka ya
Barcelona imefanikiwa kuchomoza na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Arsenal
katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya klabu bingwa
barani ulaya (UEFA) mchezo uliopigwa uwanja wa Emirates. Mabao ya
Barcelona katika mchezo huo yamefungwa na mchezaji Lionel Messi dakika
ya 71 na Dakika ya 83 likiwa ni bao la pili lililofungwa kwa njia ya
penati .
Katika mchezo mwingine Juventus wakiwa nyumbani
dhidi ya Buyern Munich, mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana
nguvu kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.Bayern Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha pili.
Kwa upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.
Michuano hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi ya Atletico Madrid.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment