Friday, 19 February 2016

Tagged Under:

Nyota wa Uganda Miya ajiunga na klabu Ubelgiji

By: Unknown On: 23:48
  • Share The Gag
  • Miya amekuwa akichezea klabu ya Vipers Sports Club
    Mchezaji nyota wa timu ya taifa ya Uganda Farouk Miya amejiunga na klabu ya Standard de Liège inayocheza ligi kuu ya Ubelgiji.
    Klabu hiyo kwa sasa imo nambari nane kwenye ligi hiyo.
    Miya amekuwa akichezea klabu ya Vipers Sports Club.
    Taarifa za awali zilikuwa zimedokeza kwamba klabu hizo mbili zimekubaliana uhamisho wake wa dola za Kimarekani 400,000 wakati akiwa bado anacheza michuano ya kombe la taifa bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani nchini Rwanda mwezi uliopita.
    Miya, 19, aliwafungia Uganda penalti na akasaidia ufungaji wa bao la pili mechi yao ya kwanza CHAN ambayo walitoka sare ya 2-2 na Mali.
    Hata hivyo, hataweza kucheza dhidi ya Zambia kama tahadhari baada yake kutatizwa na bega.
    "Kiungo wa kati mshambuliaji wa Uganda Faruku MIYA amewasili Standard de Liège Ijumaa hii! #KaribuFaruku,” klabu hiyo iliandika kwenye Twitter baada ya kuwasili kwake.
    Mchezaji huyo kwa upande wake amewashukuru watu wa familia yake na watu wengine wote waliomuunga mkono.
    “Niko tayari kwa kibarua hiki kipya,” amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.
    Msimu uliopita, Miya alifunga mabao 11 na kusaidia ufungaji wa mengine saba huku akisaidia Vipers kushinda taji la ligi kuu ya Uganda.
    Amekuwa katika klabu ya Vipers kwa miaka miwili.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment