Wizara ya Mambo ya nchi za nje
nchini Marekani imesema kwamba inatambua kwamba vifaa vya mionzi
vimeibwa kutoka katika ghala vilikohifadhiwa kusini mwa mji wa Basra
nchini Iarq.
Nchi hiyo ya Iraq iliarifu juu ya wizi huo wa vifaa
vya mionzi unaokadiriwa kufikia gramu kumi za iridium isotope mionzi
inayotumika kitabibu kupambana na ugonjwa wa kansa na kulieleza shirika
la Kimataifa la nishati za nguvu za atomiki (IAEA) mwishoni mwa mwaka wa
jana.Maofisa wa seriali nchini Iraq wanasema vifaa hivyo, vinaweza kusababisha athari kubwa kwenye mwili wa binaadamu na hata kudhuru mazingira ,lakini pia vifaa hivyo vinaweza kugeuzwa kuwa silaha ya maangamizi kama vitawafikia wanamgambo wa kundi la Islamic State au makundi mengine.
Lakini msemaji wa Wizara ya Mambo ya nchi za nje nchini Marekani , Mark Toner,amesema kwamba hakuna dalili zozote zinazoashiria kwamba wanamgambo hao wa Islamic State wanavishikilia vifaa hivyo , na kusema kwamba wataendelea kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment