Taarifa kutoka
vyombo vya habari vya somalia zinasema kuwa Waziri mkuu wa nchi
hiyo,Abdirashid Sharmarke, alishikiliwa kwa muda juzi katika kiwanja cha
ndege wa Jommo Kenyatta , Nairobi nchini kenya wakati akiwa anafanyiwa
ukaguzi wa usalama.
Taarifa hizo zinasema kuwa afisa usalama
kufanya ukaguzi kwa sababu ndege aliyokuja nayo ya kukodi ya Somalia
ilikuwa haijafanyiwa ukaguzi wa lazima katika uwanja wa ndege wa Wajir
nchini Kenya.Hata hivyo ripoti hiyo inasema ndege iliamua kuondoka na kuwaacha maafisa hao wakiwa wameshikiliwa kwa saa kadhaa.
Kenya imekuwa ikiisalidia somalia kupambana na kundi la kigaidi la la al-shabab lakini katika nchi zote mbili kumekuwa na mvutano baina ya serikali mbili juu ya kundi hilo al shabab na kusababisha mauaji ya baadhi ya askari wa kenya kuuawawa Somalia mwezi uliopita.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment