Monday, 22 February 2016

Tagged Under:

Al Qaeda,Vikosi vya Serikali vyapiga wanamgambo wa Houthi

By: Unknown On: 21:20
  • Share The Gag
  • Watu 6,000 wameuawa kutokana na mapigano nchini Yemen
    BBC imepata ushahidi kuwa vikosi vya nchini Yemen kutoka muungano wa Saudi na wanamgambo wa Al Qaeda wanapambana na waasi wa Houthi.
    Akiwa ametembelea katika mstari wa mbele wa mapigano mjini Taiz, mtengeneza makala alipiga picha za wapiganaji wa jihadi na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali,inayoungwa mkono na Wanajeshi wa jumuia ya nchi za kiarabu.
    Muungano wa majeshi kutoka nchi kumi nyingi za waarabu wa Sunni wanaiunga mkono serikali ya Yemen katika mapambano dhidi ya waasi wa kishia.
    Lakini muungano huo umekataa kuwa unashirikiana na wanamgambo wa Sunni na pia Houthi.
    Muungano wa nchi hizo umesema kuwa Al Qaeda na mitandao ya kijihadi vimekuwa vikishambulia vikosi vyake na Maafisa wa Serikali wa Yemen.
    Takriban watu 6,000 wameuawa nchini Yemen tangu mwezi March mwaka 2015, baada ya Muungano wa nchi hizo ulipoanzisha kampeni ya kijeshi kupambana na wapiganaji wa Houthi na washirika wake waliokuwa watiifu kwa Rais Ali Abdullah Saleh.
    Wapiganaji wa Houthi wanadhibiti njia zote zinazoingia na kutoka mjini na wanaudhibiti mji uliokuwa ukishikiliwa na wanamgambo wa Sunni , huku majeshi ya muungano nayo yakishambulia waasi katika maeneo ya kusini na magharibi mwa Yemen.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment