WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema agizo lilitolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli la kuwataka mawaziri ambao
hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wakamilishe kabla ya saa 12
leo jioni limetekelezwa.
Waziri
Mkuu amepokea barua kutoka kwa Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya
Viongozi wa Umma, Jaji (Mst.) Salome Kaganda ikithibitisha kuwa mawaziri
na naibu mawaziri wote wametekeleza agizo hilo.
“Hadi
kufikia saa 9.30 leo alasiri (Ijumaa, Februari 26, 2016) mawaziri wote
walikuwa wamekamilisha fomu zao za kuzikabidhi katika Ofisi za
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma,” alisema Waziri Mkuu.
Rais
Magufuli leo asubuhi alitoa maelekezo kwamba Mawaziri ambao hawajajaza
Tamko la Rasilimali na Madeni ifikapo leo Ijumaa tarehe 26 Februari,
2016 saa 12.00 jioni wawe wamejaza na kurejesha Fomu ya Tamko la
Rasilimali na Madeni katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi
wa Umma Dar es Salaam. Waziri ambaye atashindwa kutekeleza agizo hili
atakuwa amejiondoa mwenyewe kwenye nafasi yake.
Mawaziri
waliotakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilimali pamoja na hati ya
ahadi ya uadilifu kuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Charles
Kitwanga na Waziri wa Nchi (OMR – Muungano na Mazingira), Mhe. January
Makamba.
Wengine
ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano
wa Kikanda na Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga ambaye alitakiwa
kurejesha hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma na Waziri wa
Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako ambaye
alitakiwa kutoa tamko la rasilmali na madeni.
Kwa
upande wake, Naibu Waziri wa Nchi (OMR – Mazingira), Mhe. Luhaga Mpina
alitakiwa kurejesha fomu za tamko la rasilmali na madeni pamoja na hati
ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,11410 DAR ES SALAAM.
IJUMAA, FEBRUARI 26, 2016
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment