Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Butinzya, amevuliwa wadhifa huo kwa
madai ya kuchelewa kuhudhuria kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Bukombe, Amani Mwenegoha.
Utekelezaji wa kumvua madaraka mwalimu
huyo, Mathias Mazuri, ulifanywa na Ofisa Elimu Shule za Msingi wa
wilaya hiyo, Shadrack Kabanga.
Mwalimu Mazuri alichelewa kikao
kilichoitishwa na Mwenegoha Februari 6, kikiwa na lengo la kudhibiti
fedha za ruzuku ya Serikali na kwamba adhabu hiyo ni fundisho kwa
watumishi wengine.
Akitangaza kumvua wadhifa huo mbele ya walimu
wakuu wenzake, Kabanga alisema Shule ya Butinzya ipo karibu na eneo la
mkutano na wezake waliotoka mbali walifika saa 3:00 asubuhi yeye saa
6:00 mchana.
“Sikubali, huu ni muda wa kubadilika siyo kuleana,
nakuvua wadhifa kuanzia sasa siyo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi
Butinzya,” alisema.
Mwalimu Mazuri alijitetea kuwa kuchelewa
kwake kulitokana na pikipiki yake kuharibika njiani, utetezi huo
ulitupiliwa mbali na ofisa elimu.
Mkuu wa wilaya hiyo, Mwenegoha
aliwataka walimu kutumia vizuri fedha za ruzuku na kwamba,
wasichangishe wazazi kutokana na uhaba wa posho za madaraka.
Mwenegoha alipiga marufuku kuwadai wanafunzi fedha za masomo ya ziada.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment