Monday, 8 February 2016

Tagged Under:

Maelfu wauawa kinyama Syria

By: Unknown On: 21:16
  • Share The Gag
  • Ripoti ya Umoja wa Mataifa inasema maelfu ya raia wa Syria waliowekwa kizuizini wamekuwa wakifa kinyama kwa maelfu kwa kiwango kinachofikia uhalifu dhidi ya binadamu.
    Maafisa wa Umoja wa mataifa waliofanya uchunguzi huo wanasema raia wa Syria ambao wamekuwa wakiunga mkono waasi au kuipinga serikali wamekuwa wakikamatwa hapo hapo.
    Wakati huo huo Wakati Majeshi Syria yakiendelea na mapambano katika mji wa Allepo, Uturuki imesema kipaumbele chake cha kwanza ni kuwapa misaada wale waliokimbia makazi yao kutokana na vita.
    Naibu Waziri Mkuu Numan Kurtulmus amesema raia wa Syria wapatao elfu sabini na saba wanapatiwa msaada na Uturuki katika kambi katika eneo la mpakani.
    Imepangwa katika siku za usoni katika maeneo yaliyoathirika kwenye eneo hili, idadi kubwa ya wakimbizi wapatao laki sita, wanaweza kukusanyika katika eneo la mpaka wa Uturuki na Syria. kama leo karibu watu elfu sabini na saba wamepatiwa makazi kwenye kambi zilizojengwa mpakani mwa Uturuki na shirika lisilo la kiserikali la AFAD. kama unavyojua tumewachukua waarabu elfu tano na wasirya wenye asili ya Uturuki nchini Uturuki wiki iliyopita."
    Naye Waziri wa mpito wa Syria Hussein Bakri ameelezea kusikitishwa na kutokana na hali ilivyo"Haya ni mashambulizi ya mabomu yasiyo ya kawaida. Yamesababisha watu zaidi ya sabini elfu kukimbia makazi yao katika mji wa Alleppo kwa ujumla, na hasa eneo la kaskazini.Kama hali itaendelea kama hivi sasa, itasababisha watu zaidi laki nne kutoka Jimbo la Allepo na mji wa Allepo pekee kukimbia makazi yao. Ni wazi kabisa Urusi imedhamiria kuuzunguka na mji wa Allepo, kama ilivyotokea katika maeneo mengine ya Syria..





    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment