Wanafunzi
wapatao 21 wanaosoma Shule ya Msingi Kilambo cha Mkolechi, Kata ya Kala
mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, wamefukuzwa shule kwa muda
usiojulikana kwa kuvaa viatu maarufu yeboyebo.
Imeelezwa kwamba yeboyebo hizo zilikusanywa na kuchomwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kunatokana na waraka uliotolewa na Ofisa Elimu Halmashauri ya Nkasi (Msingi) ukipiga marufuku wanafunzi kuvaa aina hiyo ya viatu shuleni.
Hata
hivyo,jana Ofisa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi (Msingi), Misana
Kwangula, alikanusha kutoa waraka huo kwa shule hiyo.
“Sina
taarifa rasmi ila jana jioni (Jumatatu) alinipigia simu mkazi mmoja
akinitaarifu kwamba kuna mwalimu wa shule ya msingi Kilambo cha Mkolechi
amechoma moto viatu vya wanafunzi kwa madai kuwa ofisa elimu (msingi)
ametoa waraka kwamba wanafunzi hawatakiwi kuvaa yeboyebo shuleni…
“Hakuna
waraka wala marufuku yoyote iliyotolewa, isitoshe sio sahihi hata
kidogo wala sio kitu kizuri kuchoma vifaa walivyonavyo wanafunzi…. Sasa
kama amewachomea wanafunzi hao viatu hivyo vya yeboyebo basi awanunulie
viatu vya ngozi,” alisema Kwangula.
Mkasa
huo wa wanafunzi hao kufukuzwa shule na kuchomewa yeboyebo walizovaa
ulitokea juzi wakati wanafunzi hao walipofika shuleni wakiwa wamevaa
viatu hivyo.
Inaelezwa kwamba mwalimu wa zamu, Baraka Mwakasege aliwazuia kuingia darasani, badala yake akawaamuru wavue viatu vyao.
Taarifa
kutoka shuleni hapo zinaeleza kuwa, baada ya hatua hiyo, mwalimu huyo
wa zamu alizikusanya yeboyebo na kuzitia kiberiti kisha akawafukuza
wanafunzi hao kwa muda usiojulikana hadi wazazi na walezi
watakapowanunulia viatu vya ngozi.
Mwalimu
Mkuu wa shule hiyo, Posian Ally alikanusha kumtuma mwalimu wa zamu
kuwafukuza wanafunzi hao shule kwa muda usiojulikana wala kuteketeza kwa
moto yeboyebo zao.
Alisema
ataitisha kikao ili kujadili suala hilo na kwamba mwalimu huyo
akibainika kutenda kosa hilo ataamriwa kuwanunulia watoto hao viatu
vingine.
Credit; Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment