Walalmishi wawili
wameshindwa katika jaribio lao la kuishinikiza mahakama ya kikatiba
nchini Ujerumani kuangazia madai yao dhidi ya sheria inayopiga marufuku
kujamiiana na wanyama.
Watu hao ambao majina yao hayakutajwa wanasema kwamba wana uchu na wanyama.Walitaka kuishinikiza mahakama hiyo iliopo Karlsruhe kufikiria iwapo sheria hiyo ni kinyume na katiba.
Hatahivyo mahakama hiyo ilitupilia mbali madai yao ikisema kuwa ni haki kwa sheria hiyo kuendelea kufuatwa.
Mahakama ilisema kuwa kuwalinda wanyama dhidi ya unyanyasaji wa kingono ni jukumu la sheria ,ambayo haikubadilishwa kufuatia uamuzi wa mahakama hiyo.
Sheria za kuwalinda wanyama nchini Ujerumani zimeweka faini ya $27,700 kwa wale watakaowalazimisha wanyama kushiriki katika tabia mbaya.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment