08:44 Bw Kiggundu amesema matokeo mengine yanatarajiwa mwendo wa saa nne, lakini yanaweza yakatangazwa mapema iwapo yatakuwa tayari. Ametetea tume hiyo dhidi ya madai kwamba kura kutoka 'ngome za upinzani' hayajaripotiwa. Tume inatarajiwa kutangaza matokeo kamili kabla ya saa kumi alasiri kwa mujibu wa sheria.
08:38 Matokeo yaliyotangazwa sasa hivi ni kama ifuatavyo. Ni kutoka vituo 21,254 kutoka kwa vituo 28,010. Matokeo yaliyotangazwa yanajumuisha kura 7,822,737 ambazo ni sawa na asilimia 51,21 ya wapiga kura 15 milioni waliosajiliwa na tume hiyo. Kumbuka si wapiga kura wote waliosajiliwa ambao hufanikiwa kupiga kura.
Matokeo kwa sasa (Vituo 21,254 kati ya 28,010) | ||
---|---|---|
Abed Bwanika | 70,708 | 0.95% |
Amama Mbabazi | 112,071 | 1.50% |
Baryamureeba Venasius | 42,931 | 0.58% |
Benon Biraaro | 20,553 | 0.28% |
Kizza Besigye | 2,603,880 | 34.94% |
Joseph Mabirizi | 19,661 | 0.26% |
Maureen Kyalya | 32,773 | 0.44% |
Yoweri Museveni | 4,549,148 | 61.05% |
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) |
08:32 Kwa sasa ni wakati wa maombi Namboole, kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya kwanza ya urais ya karibuni zaidi leo.
08:28 Katibu Mkuu wa chama tawala cha NRM Justine Kasule Lumumba amekuwa akiwahutubia wanahabari kutoka Bweyogerere
Museveni anaongoza. NRM inaongoza katika kura za urais na za ubunge na tunasubiri matokeo ya mwisho. Hata kule mawaziri wameshindwa, ni watu wa kawaida. Waganda waliamua nani anafaa kuwaongoza. Kwa NRM si habari njema, lakini ni lazima tukubali.
08:13 Waangalizi wa Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuhutubia wanahabari kuhusu uchaguzi mkuu wa Uganda saa sita kasorobo.
08:10 Mwenyekiti wa EC Badru Kiggundu ameingia ukumbini kutangaza matokeo ya karibuni zaidi ya uchaguzi.
07:54 Tume ya taifa ya uchaguzi Uganda inatarajiwa kutoa matokeo mengine mwendo wa saa mbili asubuhi.
07: 52 Matokeo yaliyotangazwa kufikia sasa ni kama ifuatavyo:
Matokeo kwa sasa (Vituo 15,799 kati ya 28,010) | |
---|---|
Abed Bwanika | 51,150 |
Amama Mbabazi | 88,900 |
Baryamureeba Venasius | 33,135 |
Benon Biraaro | 15,588 |
Kizza Besigye | 1,767,041 |
Joseph Mabirizi | 14,757 |
Maureen Kyalya | 24,536 |
Yoweri Museveni | 3,156,070 |
Chanzo: Tume ya Uchaguzi Uganda (EC) |
0 comments:
Post a Comment