Wednesday, 10 February 2016

Tagged Under:

Rwanda lawamani juu ya Burundi

By: Unknown On: 22:12
  • Share The Gag
  • Rais Pierre Nkurunziza
    Maafisa wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani wamesema wameona ushahidi kuwa serikali ya Rwanda imekua ikijihusisha matukio ya machafuko katika nchi jirani ya Burundi.
    Inaelezwa kuwa Rwanda imekuwa ikiwapa silaha na mafunzo wakimbizi waliokimbia machafuko nchini Burundi.
    Burundi imetumbukia mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe tangu Rais Pierre Nkurunziza alipoamua kugombea uraisi kwa muhula wa tatu.
    Maafisa hao wa Marekani wanasema taarifa walizonazo kutoka kwa maafis wenzano waliopo kwenye kambi za wakimbizi nchini Rwanda, zinasema Rwanda imekuwa ikihusika na vurugu katika nchi jirani Burundi.
    Akihojiwa na Congress mmoja wa wanadiplomasia amesema taarifa za kuaminika kwamba wakimbizi wa Burundi ikiwa ni pamoja na watoto wamekuwa wakipewa mafunzo katika makambi nchini Rwanda, na kupambana kwa silaha na serikali.
    Ghasia zilizuka nchini Burundi mwaka jana baada ya rais wa nchi hiyo kusema atagombea kwa muhula wa tatu.
    Serikali za nchi hizi mbili zina makabila ambayo ni mahasimu , na kuna ongezeko la wasiwasi wa kimataifa kuwa mgogoro mwingine wa kikabila inaweza kuota mizizi katika eneo hilo.
    Tayari Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda amekanusha tuhuma hizo ambapo amesema Umoja wa Mataifa unapaswa kutafuta mikakati ya kutatua mgogoro ya kisiasa badala ya kutafuta nani wa kumtupia lawama.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment