Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaamini mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump hatakuwa rais wa Marekani.
Rais
Obama ameyasema hayo wakati wa mkutano mkuu wa kiuchumi wa nchi za
kusini mashariki mwa Asia unaofanyika katika jimbo la California.
''Ninaendelea kuamini kwamba Bw Trump hatakuwa rais. Na sababu ni kwamba nina imani sana na Wamarekani,” amesema Bw Obama.
Kiongozi
huyo amebainisha kuwa Wamarekani hawatampigia kura Bwn Trump kwa kuwa
wanajua kazi ya urais ni kazi kubwa si kazi ya kuongea na kuonekana
kwenye vyombo vya habari tuu.
Kwa upande wake Bwn Trump amemjibu Rais Obana na kusema kuwa hakuna mtu aliyeharibu nchi kama kipindi chake.
Mwanasiasa
huyo anamchukia sana Obama na miaka ya nyuma alizoea kumtaka atoe
stakabadhi za kuthibitisha kwamba alizaliwa Marekani.
Chanzo BBC
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment