Kiongozi mtetezi wa
demokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyi ambaye chama chake
kilishinda uchaguzi mkuu Novemba mwaka jana atateuliwa kuwa waziri.
Jina
la Suu Kyi lilikuwa kwenye orodha ya watu watakaoteuliwa mawaziri
ambayo iliwasilishwa na chama chake National League for Democracy na
kusomwa na spika wa bunge.Haijabainika atatuliwa kuhudumu katika wizara gani.
Viongozi wa zamani wa kijeshi nchini Myanmar, ambayo zamani ilifahamika kama Burma, waliingiza kifungu kwenye katiba ya nchi hiyo ambacho kinamzuia kuwa rais kwa sababu wanawe wawili wana pasipoti za Uingereza.
Mshirika wake mkuu Htin Kyaw alichaguliwa kuwa kiongozi wan chi hiyo wiki iliyopita.
Kabla ya uchaguzi, Suu Kyi alikuwa amedokeza kwamba atashiriki katika uongozi wa nchi hiyo na kusema atakuwa "juu ya rais”.
0 comments:
Post a Comment