Kufuatia
tukio la ndugu wa mgonjwa kumpiga Daktari Mkoani Mtwara, tayari jeshi
la Polisi Mkoani humo linawashikilia watu kadhaa kwa kitendo hicho cha
kumpiga Daktari wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Mtwara,Henry Mwaibambe (Pichani) amesema hadi sasa
watu 2 wanaotuhumiwa kumpiga daktari hospitali ya Mkoa wamekamatwa usiku
wa kuamkia jana wakitoroka nchini huku wengine 3 wakiendelea kusakwa.
Awali wauguzi na Madaktari wa Hospitali hiyo waligoma kufanya kazi hadi hapo watakapohakikishiwa usalama wao ndipo wafanye kazi
Jana,
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliweza kufika Hospitalini hapo na
kusuluhisha mgogoro huo huku akiomba Jeshi la Polisi kuongeza usalama
kwa watumishi hao wa Afya.
Credit;Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment