RAIS
Dk. John Magufuli kupitia Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
ametoa kiwanja chenye ukubwa wa ekari 5 kwa Bohari ya Dawa (MSD)
kilichopo Luguluni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa ajili ya
ujenzi wa Bohari ya Dawa ili kuondoa upotevu wa fedha kwa maghala ya
kukodi.
Ujenzi
wa maghala katika kiwanja hicho utaokoa kiasi cha sh. bilioni 4
zilizokuwa zikitumika kila mwaka kwa ajili ya malipo ya maghala ya
kukodi yaliyopo Mabibo Ubungo jijini pamoja na kanda mbalimbali nchini.
Akizungumza
wakati wa akikabidhi hati hiyo kwa Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean
Bwanakunu Dar es Salaam jana mchana, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, William Lukuvi alisema, Rais ametoa ardhi hiyo ili kuepusha
gharama zisizo na sababu kwa MSD.
Alisema
agizo la rais fedha zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kukodi maghala
hayo, zinapaswa kununua dawa ili kila Mtanzania apate huduma bora za
kiafya.
“Rais
aliniagiza niwape eneo, leo nimetekeleza agizo hilo kilichopo muanze
ujenzi kama mlivyoomba kwa ajili ya kujenga ghala la dawa, naamini
mtaanza mara moja balada ya kuendelea kukodi maghala na badala yake
fedha zote zitumike kwa ajili ya kununulia dawa na vifaa tiba,” alisema Lukuvi na kuongeza;
“Kiwanja
hiki ambacho kilikuwa cha Shirika la Taifa la Nyumba (NHC) kilichokuwa
na ukubwa wa ekari 200, tumewapa ekari tano kama uhitaji wenu
ulivyokuwa, nimewasamehe kodi ya premium na badala yake kiasi cha Sh16.7
hamtalipa na gharama mtakayotakiwa kulipa ni sh. milioni 2 pekee ili
muanze ujenzi mara moja.”
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Laurean Bwanakunu alisema tayari
wameshazungumza na Bodi ya wadhamini, Wizara ya Afya na wahisani hivyo
ujenzi unatarajiwa kuanza mara moja Julai Mosi.
“Tunamshukuru
sana Rais kwa sababu ombi hili limefanyiwa kazi kwa haraka sisi kama
MSD tulishindwa kuhimili mikiki kutokana na gharama kubwa iliyokuwa
ikielekezwa katika malipo ya ghala la kukodi pale ubungo mwaka wa fedha
ulioisha tulilipa kiasi cha Sh3.5 bilioni na tukitarajia mwaka huu mpya
wa fedha inafikia Sh4 bilioni kwa sababu ya malipo kwa dola,” alisema Bwanakunu.
Alisema
katika eneo hilo jipya lililopo Luguluni wanatarajia kujenga zaidi ya
maghala matano yenye ukubwa wa sikwea mita mita 5000 yatakayogharimu
kiasi cha sh. bilioni 10 kila mojawapo, ujenzi huu utakapokamilika kanda
zitakazonufaika ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro na Pwani na kuwa
eneo hilo walilopata wanaweza kujenga kiwanda cha maji.
Credit;Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment