Rais Barack Obama na mwenyeji wake
Raul Castrol wamejibizana kuhusu suala la haki za binadamu na vikwazo
vya kibiashara baina ya Marekani na Cuba.
Katika siku ya pili ya ziara yake ya Kihisitoria nchini Cuba, rais Obama amesema kuondolewa kwa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo la Kikomonisti kutategemeana na uharaka wa mataifa hayo mawili kuondoa tofauti zao hasa katika suala la haki za binadamu.
Obama amesema kuwa Marekani haioni kama Cuba ni tishio kwa Marekani na kwamba ziara yake nchini humo ina lengo la kuweka misingi mipya kati ya mahusiano baina ya nchi hizo mbili.
Rais Obama baada ya mazungumzo ya mjini Havana na mwenyeji wake Raul Castro, amesema kutokuwepo harakati za kupigania haki za binadamu nchini Cuba ni jambo litakalo mpatia ugumu kushawishi bunge la Congress kuondoa vikwazo vilivyopo dhidi ya Cuba.
0 comments:
Post a Comment