Mbunge
wa Kigamboni, Dar es Salaam ,Faustine Ndugalile (CCM) amekosoa utendaji
wa mawaziri wa serikali ya Rais Magufuli akisema wanatishia
wafanyakazi badala ya kuwaelekeza katika utendaji wao.
Katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wa twitter kwa lugha ya kiingereza, Ndugalile ameandika: "Ministers
should encourage or provide practical solutions to problems instead of
barking orders and terrorizing civil servants."
Kwa lugha ya kiswahili, mbunge huyo alimaanisha:" Mawaziri wanatakiwa kuwatia moyo au kutoa suluhisho kwa matatizo badala ya kufoka na kuwatisha watumishi wa umma."
Alipoulizwa kuhusu ujumbe huo,Ndugalile alikiri kuwa ni wake na kusisitiza kuwa ni wajibu wake kama mbunge kuisimamia serikali.
"Mimi ni mbunge, kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali.Ikifanya vizuri tutaisifia, ikikosea tutaikosoa.
"Nimesema baadhi ya mawaziri- sio wote wanawatisha wafanyakazi. Kazi ya kiongozi ni kuonyesha uongozi na si kuwa bosi.
"Inaonyesha kuna baadhi ya mawaziri wamekuwa kila kitu ;wao ndo mawaziri,ndo wakurugenzi, ndo wakuu wa idara..." alisema
Ndugalile
anakuwa mbunge wa kwanza wa CCM kukosoa kasi ya mawaziri wa Rais
Magufuli, huku mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akimkosoa Rais
Magufuli kwa kuwasimamisha baadhi ya watendaji wa serikali bila kufuata
taratibu za utumishi wa umma na sheria za kazi.
Akifafanua
zaidi, Ndugalile alisema baadhi ya mawaziri wamekuwa wakitoa amri
zisizotekelezeka na zinazotofautiana na ilani ya uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2015.
"Kuna
baadhi ya mawaziri wanatoa amri zisizotekelezeka.Kwa mfano, mtu anatoa
amri itekelezwe ndani ya siku 3, itawezekanaje? umewapa rasilimali za
kutekeleza?" alihoji Ndugalile.
Hata hivyo, Ndugalile alisema anaunga mkono hatua za kudumisha nidhamu kwa watumishi wa umma zinazofanywa na mawaziri.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment