Sunday, 27 March 2016

Tagged Under:

Boko Haram Wateka Wanawake Wengine 16

By: Unknown On: 22:28
  • Share The Gag

  • Wapiganaji wa Kundi la Boko Haram wamewateka nyara wanawake 16 katika eneo la mashambani, Kaskazini Mashariki mwa Jimbo la Adamawa.

    Vyanzo vya habari vilisema wanawake hao walitekwa msituni, walipokuwa wakitafuta kuni na wengine walikuwa wakivua samaki kando ya mto.

    Wanawake hao hadi sasa hawafahamiki mahali walipohifadhiwa na watekaji.

    Kundi hilo lililoenea nchini humo, limekuwa likijihusisha na vitendo vya utekaji wa mara kwa mara. Awali, liliwateka wasichana ambao ni wanafunzi zaidi ya 200 ambao mpaka sasa hawajapatikana.

    Wakati huohuo, Jeshi la Nigeria limewakomboa zaidi ya watu 800, waliokuwa wakishikiliwa na kundi hilo katika vijiji kadhaa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

    Mateka wengine walikombolewa katika Jimbo la Borno, huku 520 wakikombolewa katika Kijiji cha Kisuma, baada ya mapambano kati ya wanajeshi hao na wapiganaji wa kundi hilo, mateka wengine 309 waliokolewa katika vijiji vingine 11 vinavyodhibitiwa na kundi hilo.

    Rais wa nchi hiyo, Muhammadu Buhari alipokuwa anaingia madarakani alisema atahakikisha anapambana na kundi hilo
    ==
    Credit; Mpekuzi Blog 

    0 comments:

    Post a Comment