Siku tatu baada ya kuibuka kwa kashfa ya rushwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemuita Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kumhoji.
Muda
mfupi baada ya taarifa za kashfa hiyo kuwa wazi, Zitto na mwenzake wa
Nzega Mjini, Hussein Bashe ambao ni wajumbe wa Kamati ya Huduma za
Jamii, walimuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiondoa kwenye
nafasi zao ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo.
Zitto
alithibitisha kupata wito kutoka makao makuu ya Takukuru ili kuhojiwa
juu ya sakata hilo na akapongeza kuwa endapo vyombo vya Serikali
vitakuwa makini kushughulikia tuhuma zote zinazoelekezwa kwa wanasiasa
na watumishi wengine wa umma, itasaidia kuongeza uwajibikaji na
kupunguza uzushi kwa wananchi.
“Nimepata
wito huo kupitia Ofisi ya Bunge. Nasikia Bashe ameitwa pia. Nafurahi
wito wetu wa uchunguzi umechukuliwa kwa uzito unaostahili na tutatoa
ushirikiano wote kwa vyombo vya uchunguzi ili kumaliza zoezi hili kwa
haraka na kwa ufanisi,” alisema Zitto.
Alipotafutwa Bashe ili kupata ukweli wa kuitwa kwake, ingawa hakutimiza ahadi yake, alisema:“Sipo kwenye nafasi nzuri ya kuzungumza hivi sasa.”
Mpaka
jana, wakati Takukuru ikiendelea kuwahoji wanasiasa na watendaji wa
mashirika yaliyotajwa kuhusika kutoa rushwa ili kubadili maoni ya
wajumbe juu ya utendaji wao, wabunge wawili walithibitika kuitwa na
Takukuru.
Tuhuma
hizo zimekwenda sambamba na Ndugai kuwaondoa wenyeviti wa kamati za
Ardhi, Maliasili na Utalii; Nishati Madini; Uwekezaji na Mitaji ya Umma
huku ile ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na Huduma na Maendeleo ya
Jamii lakini akisema ni uhamisho wa kawaida
Mkurugenzi
Mkuu wa Taakukuru, Valentino Mlowola, bila kuingilia uchunguzi
unaoendelea alithibitisha kuwaita wabunge hao na watendaji wa mashirika
waliohojiwa.
“Hili
ni suala la uchunguzi Bado linaendelea hivyo si wakati muafaka kutaja
watu waliohojiwa mpaka sasa ingawa mahojiano yanaendelea. Kazi
ikikamilika utapata taarifa kamili,” alissema Mlowola.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment