Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao ambapo jana alimtembelea Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar
es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwa ajili ya kupata baraka na busara zake
Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam.
Mkuu
huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili
afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo
kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya
kisasa.
Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo
ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika
utendaji wake.
“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kwa mujibu wa
mkuu huyo wa mkoa, leo anatarajia kukutana na Mufti Mkuu wa Tanzania,
Sheikh Abubakary Zubeiry na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa
Salum.
Kadinali
Pengo akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda ofisini kwake makao makuu ya Kanisa Katoliki, Forodhani jijini
jana
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment