Wednesday, 23 March 2016

Tagged Under:

Mshukiwa wa Brussels aliunda mabomu ya Paris

By: Unknown On: 22:48
  • Share The Gag
  • Watu wengi walijeruhiwa kwenye mashambulio hayo
    Maafisa wa Ufaransa na Ubelgiji wanasema mmoja wa walipuaji wa kujitoa mhanga waliotekeleza mashambulio ya Brussels alikuwa mtaalamu wa kutengeneza mabomu.
    Wamesema mshukiwa huyo alihusika katika kuunda mabomu yaliyotumiwa kutekeleza mashambulio ya Paris Novemba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 130.
    Wakizungumza, bila kutaka kunukuliwa, maafisa hao walisema chembe nasaba za DNA za mshukiwa huyo Najim Laachraoui zilipatikana katika mikanda ya kujilipua iliyotumiwa Paris.
    Hajatambuliwa rasmi hata hivyo.
    Watu 34 walifariki na wengine wengi kujeruhiwa kwenye mashambulio yaliyotekelezwa uwanja wa ndege wa Zaventem na kituo cha treni cha Maelbeek.
    Najim Laachraoui Kundi la Islamic State limedai kutekeleza mashambulio hayo.
    Msako mkubwa unaendelea kumsaka mshambuliaji ambaye hajatambuliwa na ambaye anaaminika kutoroka.
    Washambuliaji wawili wametambuliwa kama ndugu Khalid na Brahim el-Bakraoui.

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment