Majeshi ya Sudan
yamepambana na waasi wa SPLM kaskazini katika eneo la Kordifan ya Kusini
baada ya miezi kadhaa ya utulivu katika eneo hilo.
Taarifa zinasema kumekuwa na mapigano makali katika eneo la Karkaraya.Msemaji wa chama cha SPLM kaskazini amesema wamechukua udhibiti, huku majeshi ya serikali yakisema yamewarudisha nyuma waasi kwa mashambulizi.
Kutokana na eneo hilo kutofikika imekuwa vigumu kuthibitisha taarifa ambzo zimekuwa zikikinzana kuhusu mgogoro huo ambao umekuwa ukiendelea tangu mwaka 2011.
Katika taaarifa iliyotolewa na msemaji wa waasi wa SPLM Kaskazini Arnu Lodi amethibitisha kuwepo kwa mapigano ambayo yamekuwa yakiendelea katika eneo la Karkaraya na Agab Kordofan ya Kusini.
Msemaji huyo amesema wamedhibiti eneo hilo na kwamba hakuna majeruhi kwa upande wao waliotokana na operesheni hiyo.
Naye msemaji wa majeshi ya serikali ya Sudani Bregedia Ahmed Khalifa ameongea na AFP kwa njia ya simu ambapo amesema siku ya jumanne kundi kubwa la waasi liliingia katika mji wa Um Serbida na kushambulia eneo la Karkaraya uliokuwa chini ya udhibiti wa majeshi ya serikali.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment