Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro
POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imebaini mtandao wa wezi wa
magari baada ya kukamata watu 50 sanjari na kupata magari 24 yaliyoibwa
na kusafirishwa kwenda kwenye baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro
aliwaambia waandishi wa habari kwamba, magari hayo yamekuwa yakiibwa kwa
kutumia mbinu mbalimbali, ikiwemo funguo bandia na kisha kubadili
chesisi.
Alitaja mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyanga na Kagera kuwa sehemu
ambazo magari hayo ya wizi yamekuwa yakisafirishwa kwenda kufichwa kabla
ya kuuzwa kwa watu mbalimbali.
Wakati baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa jijini Dar es Salaam wakiwa
safarini kusafirisha magari hayo ya wizi, mengine yamekutwa kwenye
maeneo hayo yakiwa yameshauzwa.
Sirro, ambaye alikuwa akizungumzia operesheni za usalama
zinazoendelea mkoani Dar es Salaam, alitaja baadhi ya watuhumiwa pamoja
na namba za baadhi ya magari yaliyopatikana baada ya polisi kufuatilia.
Alisema Februari 15, mwaka huu, mtuhumiwa Charles Simon (34) mkazi wa
Mabibo ambaye ni dereva teksi, alikamatwa maeneo ya Kimara akidaiwa
kusafirisha gari la wizi aina ya Fuso kwenda mkoani Mwanza.
“Magari wanayoyaiba, wamekuwa wakiyapeleka mafichoni katika mikoa ya
Kanda ya Ziwa hasa Mwanza, Geita, Shinyanga na Kagera,” alisema Kamanda
Sirro. Alitaja tukio lingine ni la Februari 15 mkoani Shinyanga katika
eneo la Magereji ambako kamanda alimtaja mtuhumiwa Isack Kahwa (35) kuwa
alikutwa na gari ya wizi iliyobainika mmiliki wake ni mkazi wa Tabata
Segerea, Dar es Salaam, Erick Senzotz.
Kamanda alimtaja mtuhumiwa Kahwa kuwa ni Mkazi wa Ndala na fundi
magari. Gari hilo linalodaiwa kuwa ni la wizi mali ya Erick, ni aina ya
Toyota IST yenye namba T428 CYV rangi nyeupe. Inadaiwa mtuhumiwa huyo
alikiri kuuza magari mengine.
Magari mengine ya wizi ambayo yalishauzwa ni Toyota Noah yenye namba
T948 DCP, iliyokamatwa wilayani Mbogwe katika Mji wa Masumbwe mkoani
Geita; likiwa limeuzwa kwa Sadiki Masele. Kwa mujibu wa kamanda,
upelelezi umebaini kuwa gari hilo liliibwa maeneo ya Kimara, Dar es
Salaam likiwa na namba ya usajili T799 DEU.
Kamanda alisema magari mengine yaliyokamatwa ni lenye namba za
usajili T702 CMS Toyota Hiace iliyokamatwa Kahama akiwa nayo Victor
Malya (38). Nyingine ni Toyota Noah yenye namba T419 iliyokamatwa
Shinyanga Madukani akiwa nayo Adrian Jackson (45).
Magari mengine yaliyoibwa Dar es Salaam na maeneo yalikokutwa kwenye
mabano ni Toyota Carina TI namba T185 BHK (Kandoto, Shinyanga), Toyota
Noah T227 CNB (Shinyanga), Toyota Noah T445 CEN (Shinyanga), Toyota Noah
T481 CFU, T778 CPB Toyota Noah.
Mengine yaliyoibwa Dar es Salaam kwa nyakati tofauti na kukutwa
mkoani Shinyanga ni T289 CPP Toyota Noah , T369 CRM Toyota Verossa, T270
DBX Toyota Noah, T965 BLG Toyota RAV4, T462 CMA Toyota IST, T331 Toyota
RAV4, T793 BHB Toyota Noah, T859 DCZ Fuso, T227 CKQ Toyota IST, T334
CCY Toyota Spacio, T556 CTX Toyota IST na T437 BMJ Toyota Carina.
Chanzo HabariLeo.
Monday, 14 March 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment