Kumekuwa na milio
ya risasi katika maeneo mbali mbali ya mji wa mkuu wa Libya Tripoli
kufuatia kuwasili kwa njia ya bahari Waziri Mkuu Fayez Seraj pamoja na
mafaasa wengine wa serikali ya Umoja wa Kitaifa inayoungwa mkono na
Umoja wa mataifa.
Kituo cha televisheni cha libya Al Naab kimefungwa na kimezuiwa kutangaza ambapo pia makao makuu yake yameshambuliwa na watu wenye silaha.
Mamlaka iliyojitangazia utawala katika mji mkuu wa Tripoli wamekuwa wakisema mipango inayofanywa na baraza la rais ni jaribio la mapinduzi ambapo baadhi wamesema watu hao wakamatwe.
Katika mkutano na waandishi wa habari katika ngome ya kikosi cha majeshi ya majini Waziri Mkuu Fayez Seraj amesema huu ni mwanzo wa ukurasa mpya.
"Tunamshukuru Mungu tumefika salama hapa Tripoli pamoja na changamoto tulizokutana nazo. Mpango wetu ni kuunganisha walibya pamoja na kuwepo kwa mpasuko. Vijana wetu ndio watakaoijenga Libya na kuipigania. Mungu atubariki sote." Alisema.
Nayo Wazara ya Mambo ya nje ya Marekani imetoa wito kwa pande zote nchini Libya kufanya kazi pamoja na kutafuta suluhisho ya mvutano wa kisasia. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje John Kirby amesema pande zote zinapaswa kufanya na kutafuta mstakabali wa amani ya Libya.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment