Tuesday, 29 March 2016

Tagged Under:

Rais Rousseff hatarini kuondolewa madarakani

By: Unknown On: 22:33
  • Share The Gag
  • Rais wa Brazil Dilma Rousseff
    Serikali ya umoja wa kitaifa ya Brazil imepata pigo baada ya kujiondoa kwa chama mshirika cha PMDB. Mawaziri kutoka chama PMDB sasa itabidi wajiuzulu pamoja na watendaji wapatao mia sita walioteuliwa na serikali.
    Kujiondoa kwa chama hicho sasa kunamweka pabaya Rais Dilma Roussef katika hatari ya kuondolewa madarakani na bunge.
    Makamu wa Rais wa chama cha PMDB Romero Juca yeye ndio aliyetangaza uamuzi huo chama hicho kujiondoa.
    "Kuanzia leo na kuendelea katika mkutano huu wa kiistoria wa PMDB, PMDB inajiondoa katika serikali ya Rais Dilma Rouseff." amesema Romero
    Kwa upande wake msaidizi wa kiongozi wa upinzani Bungeni kutoka PMDB Leonardo Quintao wafanyabiasha wamekosa imani na Rais.
    "Kila sekta ya uzalishaji nchini Brazil na vsekta ya fedha nchini Brazil, zimetoa taarifa zikisema wanajiondoa kuumuunga mkono Rais wa Brazil Dilma Rouseff, kwa sababu watu wanapoteza ajira. Mwaka jana karibu wabrazil milion moja nukta tano walipoteza ajira kwa sababu hawakuwa tayari kuwekeza nchini Brazil kutokana na jinsi Rais anavyoongoza serikali."


    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment