Wakati
waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tamisemi na utawala bora George
Simbachawene akitoa muda wa uchaguzi wa mameya kukamilika ifikapo machi
25 mwaka huu,Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam,
Juma Simba “Gadafi” amemuomba Waziri huyo kuangalia upya utendaji kazi
wa wakurugenzi wa Manispaa za Ilala na Kinondoni, akidai wamevuruga
uchaguzi wa meya na naibu wake.
Akizungumza
na wanahabari jana, Simba alisema CCM imefikia hatua hiyo baada ya
kutoridhishwa na utendaji kazi wa wakurugenzi hao, ikiwamo kushindwa
kutafsiri vyema vifungu vya sheria vilivyosababisha kuondolewa kwa
majina ya wajumbe wao kwa madai kuwa hawana sifa za kushiriki uchaguzi
huo.
“Wakurugenzi
hawakuwa majasiri katika kupambana na vitisho vya wajumbe wa Ukawa na
kuwa wakweli. Walishindwa kutoa tafsiri sahihi ya wajumbe halali
wanaotakiwa kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa jiji,” alilalamika Gadafi.
Kwenye
mkutano huo Gadafi alidai kwamba wakurugenzi hao walifanya upotoshaji
wa tafsiri sahihi kuhusu uwepo wa wajumbe wa CCM walioonekana kutokuwa
wajumbe halali.
“CCM imesikitishwa na upotoshaji uliofanywa na wakurugenzi hao hasa kwa kuwavua uhalali wa kupiga kura baadhi ya wajumbe wetu,” alisemea na kuongeza;
“Wakurugenzi
wa Manispaa za Ilala na Kinondoni wamekula matapishi yao, haiwezekani
uchaguzi wa awali wawakubali wabunge viti maalum kama wajumbe halafu
uchaguzi wa jiji waseme hawastahili kupiga kura.”
Gaddafi
alidai kwamba, Ukawa ndio walikuwa wa kwanza kuuvuruga uchaguzi huo kwa
kuwa walitumia njia ya vitisho na kuwafanya wakurugenzi wafanye maamuzi
kulingana na mashinikizo yao.
Alidai
kwamba, licha ya CCM kuonekana kuwa chanzo cha kuvuruga uchaguzi huo
lakini chama hicho hakina sababu hata moja ya kufanya hivyo isipokuwa ni
utaratibu wanaoshinikiza ufuatwe na kuwa wana mgombea bora na
anayekubalika.
“Wajumbe
wa Ukawa ndiyo walianza kukiuka taratibu za upigaji kura kwa kupiga
picha kura walizopiga na kumuonesha mmoja kati ya viongozi wao.
“Uchaguzi
hupigwa kwa siri, iweje Ukawa wawalazimishe wajumbe wao kupiga picha
kura walizopiga? Ina maana wanaogopa wajumbe wao wasije wakaipigia kura
CCM,”alisema.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment