Saturday, 12 March 2016

Tagged Under:

Maambukizi ya Ukimwi bado juu

By: Unknown On: 22:10
  • Share The Gag

  • Wabunge Kamati ya Ukimwi wakiwa katika kikao cha kuzungumzia mambo mbalimbali yanayohusu Ukimwi Dar es Salaam jana. (Picha na Yusuf Badi).

    MAKAMU Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi na dawa za kulevya Kanyasu John amesema kampeni ya masuala ya Ukimwi hivi sasa imepungua kasi japo maambukizi katika baadhi ya maeneo bado yapo juu.
    John ambaye pia ni Mbunge wa Geita Mjini alisema jana wakati wa semina elekezi iliyokuwa ikitolewa na Mradi wa Kujengea Uwezo Wabunge na Watumishi, jijini Dar es Salaam. Alitaka kampeni hizo zilizoanzishwa na serikali zisilale bali kila mmoja ajitahidi kufanya uhamasishaji ili ugonjwa huo usiendelee kuenea kwa wale ambao hawajapata maambukizi.
    Kwa upande mwingine alisema semina hiyo wanaipata kwa wakati kwa kuwa karibu asilimia 90 ya wabunge ni wapya, hivyo wanajengewa uwezo wa kamati hiyo na kuongeza kuwa walipoteuliwa kwenye kamati hiyo walijiona kama hawana majukumu makubwa ya kufanya, hivyo semina hiyo itapanua mawazo yao na kujua majukumu yao hasa ni yapi.
    Alitaja baadhi ya mada walizofundishwa kuwa ni uanzishwaji wa sheria, utungaji wa sheria pamoja na wajibu wa kamati hiyo. Kwa upande wake Mtaalamu wa Ukimwi na Afya kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Dk Bwijo Bwijo alisema kuwa tangu mgonjwa wa kwanza atambulike nchini miaka ya 1980 hadi leo kuna mafanikio na changamoto nyingi ambazo serikali inakabiliana nazo kwa lengo la kutokomeza ugonjwa huo.

    Chanzo HabariLeo.

    0 comments:

    Post a Comment