Mgombea Urais katika chama cha
Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa akichaguliwa kuwa
Rais hatua ya kwanza atakayochukua juu ya masuala ya kigeni ni
kuvunjilia mbali mkataba wa Nyukilia.
Mkataba huo ambao Trump anauzungumzia na kukerwa nao ni ule wa Marekani na Iran.Bwana Trump, ambaye kwa sasa yuko mstari wa mbele katika kinyang'anyiro hicho katika chama chake aliliambia kundi lenye ushawishi mkubwa linalounga mkono Israel kuwa mapatano hayo ya Iran ni hatari kwa Marekani.
Amesema pamoja na madhara kwa Marekani lakini pia unaweza kuihatarisha Israel na Mashariki ya Kati.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment