Tuesday, 15 March 2016

Tagged Under:

Serikali Ya Tanzania Yalilia Meno ya Tembo Yaliyochomwa Moto nchini Malawi

By: Unknown On: 22:06
  • Share The Gag

  • Serikali imeanza mazungumzo na Ubalozi wa Malawi nchini baada ya nchi hiyo kuteketeza tani 2.6 za meno ya tembo yaliyotoka Tanzania. 
     
    Serikali inafanya mazungumzo hayo ili kuzuia kuchomwa kwa meno mengine yaliyopo nchini humo kwa kuwa ni kielelezo kinachohitajika mahakamani.

    Mkurugenzi wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Herman Keraryo alisema mwanasheria wa wizara alifanya mawasiliano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ubalozi huo ili kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Malawi. 

    Idadi ya vipande vya meno ya tembo vilivyokamatwa nchini  Malawi ni 781 na thamani yake inakisiwa kuwa  bilioni 3. 

    Katika hatua nyingine; Serikali ya Kenya inatarajia kuteketeza tani 120 za meno ya tembo mwishoni mwa mwezi huu baada ya kuyakamata nchini humo. 
    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    0 comments:

    Post a Comment