Idara ya Haki ya
Marekani imesema huenda shirika la upelelezi la FBI limegundua njia ya
kufungua simu ya mkononi ya muuaji aliyewapiga risasi watu eneo la San
Bernardino, Syed Rizwan Farook.
Idara hiyo imeiomba mahakama
kuahirisha kusikilizwa kwa kesi kati ya shirika hilo dhidi ya kampuni ya
utengenezaji wa simu, Apple.Idara hiyo imekuwa ikishawishi mahakama ilazimishe Apple kufungua simu ya Farook, ambaye yeye na mkewe wanatuhumiwa kufanya shambulizi la bunduki na kuwaua zaidi ya watu 14 katika jimbo la California, Desemba, mwaka jana.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment