Wednesday, 23 March 2016

Tagged Under:

Mchina akiri kuiba siri za Marekani

By: Unknown On: 22:49
  • Share The Gag
  • Miongoni mwa siri nyingine, Su na wenzake walisaka siri kuhusu ndege aina ya F-22
    Mwanamume mmoja kutoka Uchina amekiri kuhusika katika njama ya kuiba siri kuu kuhusu mifumo ya kijeshi ya Marekani.
    Su Bin anaaminika kuwa kwenye kundi la watu ambao wamekuwa wakiiba habari kuhusu ndege za kivita, ndege za kubeba mizigo na silaha.
    Wizara ya haki ya Marekani imesema kupitia taarifa kwamba Bw Su alilenga kufaidi kifedha.
    Bw Su, mwenye umri wa miaka 50, alikamatwa akifanya kazi nchini Canada mwaka 2014.
    Alidaiwa kuwa na kampuni ya Kichina ya teknolojia ya uchukuzi wa ndege iliyokuwa na afisi Canada na alikamatwa akijaribu kupata uraia wa Canada.
    Alikiri kufanya kazi na watu wawili kutoka Uchina kati ya Oktoba 2008 na Machi 2014 kudukua mifumo ya kompyuta ya Marekani, ikiwemo kampuni ya Boeing inayotumiwa na jeshi la Marekani kuunda ndege zake.
    Sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka mitano jela na faini ya $250,000 (£170,000).

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment