Ikulu ya Marekani imeiambia BBC kuwa
Marekani inathamini sana uhusiano wake na Uingereza ,hayo yalisemwa saa
chache baada ya Rais Obama kuikosoa vikali sera ya mambo ya nje ya
Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron.
Rais Obama aliliambia
jarida la "The Atlantic"kuwa Uingereza na Ufaransa walisababisha Libya
kufikia katika hali mbaya baada ya majeshi yao kuingilia kati.Hata hivyo BBC imepokea maelezo mengine kutoka Marekani kupitia msemaji wa Ikulu Ned Price yanayomsifu Cameron kwa uongozi wake wa jumuiya ya kijeshi ya nchi za magharibi NATO.
Mhariri wa BBC America ya kaskazini amesema uongozi wa Obama unaonekana kuwa katika mkanganyiko mkubwa.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment