TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
ziara ya kushitukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja
na mambo mengine ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa
malimbikizo ya malipo ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na
badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa
uhakiki.
Mpaka Rais Magufuli anatoa agizo hilo, Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini ya kufanyika malipo.
Akizungumza
na watendaji wakuu wa Benki Kuu ya Tanzania waliojumuisha Gavana, Naibu
Magavana, Wakurugenzi na Mameneja, Rais Magufuli ametaka Wizara ya
Fedha ifanye upya uhakiki wa malipo hayo, ili kubaini kama walengwa
walioidhinishwa kulipwa wanastahili kulipwa ama vinginevyo.
Aidha,
Dkt. Magufuli ameagiza Kitengo cha madeni ya nje ambacho awali kilikuwa
chini ya Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe
Benki Kuu mara moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa
madeni.
Wakati
huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Gavana wa Benki Kuu
ya Tanzania Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki
hiyo, na kuwaondoa mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa
wafanyakazi katika benki hiyo.
"Haiwezekani tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi wanazofanya hazijulikani" Amesema Dkt. Magufuli.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati ambapo Benki Kuu ya Tanzania ina wafanyakazi 1391.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam-10 Machi, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
akiwa kaongozana na Naibu Gavana wa BOT Dkt Natu Mwamba akiwasili makao
makuu ya Benki Kuu ya Tanzania alikofanya ziara ya kushtukiza leo Machi
10, 2016.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akizungumza na ungozi wa juu wa Benki Kuu ya Tanzania ambao ameupa
maelekezo mbalimbali katika kuboresha utendaji wao wa kazi wakila siku.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akikagua CV za wafanyakazi wa Benki Kuu ya Tanzania wakati wa ziara
yake ya kushtukiza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Gavana wa Benki
Kuu Beno Ndulu.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment