SIMBA jana imetema ubingwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya
kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar. Katika mechi hiyo
iliyochezwa kwenye uwanja wa Amaan mjini hapa, Simba ilionekana kutawala
karibu muda mwingi wa mchezo lakini washambuliaji wake mara kadhaa
walikosa mabao ya wazi.
Ibrahim Jeba ndiye aliyefunga bao hilo pekee katika mechi hiyo ya
jana na kuimaliza Simba iliyotamba kutetea taji lake. Jeba alifunga bao
katika dakika ya 45 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa
Simba Peter Manyika.
Simba ilianza kipindi cha pili kwa kufanya mabadiliko ambapo iliwatoa
Mussa Hassan Mgosi, Emily Nimuboma na Awadh Juma na nafasi zao
kuchukuliwa na Brian Majegwa, Ibrahim Ahibu na Said Ndemla. Hata hivyo
mabadiliko hayo hayakuisaidia Simba zaidi ya washambuliaji wake kukosa
mabao mara kwa mara.
Dakika ya 75 Daniel Lyanga alikosa bao baada ya kubaki peke yake na
kipa Said Mohammed lakini alipiga vibaya mpira ukapanguliwa na kipa
huyo. Zikiwa zimesalia dakika za nyongeza Abdi Banda alikosa bao lingine
la wazi baada ya kubaki peke yake na kipa lakini akapaisha.
Mtibwa sasa inatarajiwa kucheza fainali keshokutwa na mshindi wa
mechi kati ya Yanga na URA ya Uganda iliyotarajiwa kuchezwa jana usiku.
Created by Gazeti la habariLeo.
Monday, 11 January 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment