Na Elias Msuya, Dodoma
TANZANIA inakabiliwa na upungufu mkubwa wa watumishi wa afya, hali
inayochangia vifo kwa wagonjwa wengi kutokana na kukosa huduma.
Akiwasilisha mkakati wa kuboresha rasilimali watu katika sekta ya
afya nchini, kwa wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii na Maendeleo ya
Jamii, Meneja wa Mipango na Utetezi wa Sera kutoka Taasisi ya Benjamin
Mkapa, Manka Kway, alisema mwaka 2014-15 kulikuwa na mahitaji ya
madaktari wasaidizi 1,744, lakini waliopatikana ni 149 tu.
Alisema tathmini hiyo imefanyika wilaya 30 za mikoa saba ya Tanzania
ambayo ni Geita (Bukombe na Chato), Iringa (Kilolo, Mafinga, Iringa,
Mufindi), Kilimanjaro (Mwanga, Siha, Rombo, Hai, Moshi na Moshi
Manispaa).
Mikoa mingine ni Mtwara (Tandahimba, Masasi, Mtwara, Manispaa ya
Mtwara), Pwani (Kisarawe, Rufiji, Bagamoyo, Kibaha na Mji wa Kibaha),
Ruvuma (Mbinga, Namtumbo, Songea na Mji wa Songea), Shinyanga (Shinyanga
Manispaa na Halmashauri ya Shinyanga).
“Mahitaji ya madaktari wasaidizi kwa mwaka 2014-15 yalikuwa 1,744,
waliokuwapo ni 149 na waliopungua 1,595 sawa na asilimia 91,” alisema
Kway.
Mbali na madaktari wasaidizi, alisema kuna upungufu wa maofisa
wauguzi kwa asilimia 33, maofisa tabibu wasaidizi kwa asilimia 78,
maofisa tabibu kwa asilimia 26, wauguzi kwa asilimia 72, maofisa wauguzi
kwa asilimia 53 na wataalamu wa maabara kwa asilimia 37.
“Sekta ya afya inakabiliwa na uhaba wa rasilimali watu kwa asilimia
52 kupitia ikama ya mwaka 2014…zaidi ya asilimia 74 ya madaktari waliopo
wanafanya kazi maeneo ya mijini… wakati daktari mmoja anahudumia
wagonjwa 78,880 maeneo ya vijijini, daktari mmoja mijini anahudumia
wagonjwa 9,095. Shirika la Afya Duniani (WHO) linaelekeza uwiano wa
1:10,000,” alisema Kway.
Baadhi ya wabunge wakichangia maoni kuhusu tathmini hiyo, waliitaka
Serikali kurekebisha sera na sheria zake ili kuweka mazingira wezeshi
kwa watumishi wa afya kufanya kazi vijijini.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alisema sera ya afya
inayowezesha madaktari wa mijini kulipwa zaidi ya wanaofanya kazi
vijijini ni kikwazo kwao kwenda vijijini.
“Kwanini mhitimu wa shahada ya udaktari akiajiriwa Hospitali ya Taifa
Muhimbili au Mwananyamala analipwa mshahara mkubwa kuliko yule
anayefanya kazi Wilaya ya Nzega?” alihoji Bashe.
Alisema tatizo hata bajeti ya afya inapopitishwa bungeni huwa
haifikishwi yote, hivyo akawataka wabunge kusimamia bajeti hiyo itolewe
kikamilifu.
Naye Mbunge wa Urambo Mashariki, Margaret Sitta, alisema ili
watumishi wa afya waende vijijini ni vema wapewe mafao ya kuwa huko.
Chanzo Mtanzania
Sunday, 31 January 2016
Wamasai kuchumbia mimba ni ukatili
By:
Unknown
On: 23:30
Wanawake wa kimasai wakiimba. Baadhi yao walichumbiwa wakiwa tumboni mwa mama zao, hali ambayo iliwanyima uhuru wa kuchagua mume wanayemtaka na hata kupata elimu. |
KUNA mila na desturi potofu katika jamii mbalimbali zinazosababisha ukatili wa kijinsia kwa wasichana katika wilaya ya Simanjiro. Jamii ya kimasai imekuwa ni miongoni mwa makabila yenye mila kandamizi kwa mtoto wa kike.
Katika kabila hilo, mtoto wa kike hana haki na hathaminiwi kama yule wa kiume ikiwa ni pamoja na suala zima la kupata elimu. Ofisa Elimu Shule za Msingi wilayani Simanjiro, Silvanus Tairo anasema, kitendo cha kutoandikisha watoto wote wa kike wenye umri wa kwenda shule ni ukatili wa kijinsia kwa kuwa kinawanyima fursa ya kujengewa uwezo wa kujitegemea.
Utamaduni wa wanaume kuhitaji kuoa wanawake waliokeketwa ni ukatili mwingine katika kabila la Wamasai. Inadaiwa kwamba, katika kabila hilo, ili msichana aolewe moja ya sifa ni lazima awe amekuzwa kimaumbile kwa maana ya sehemu za siri tangu akiwa mdogo kwa kuwekewa vidole au vijiti na mama au bibi yake. Inasemekana kwamba, maumbile hayo yakikuzwa yanamrahisishia mwanamume asipate shida atakapomwingilia mwanamke huyo.
“Anafanyiwa hivyo na mama au bibi yake ili akipelekwa kwa mume asipate tabu kwa kuwa mama anakuwa amefanya kazi yake,” anasema mmoja wa wakazi wa huko. Kutokana na utamaduni huo, kuna tatizo la utasa kwa Wamasai linalotokana na vitendo hivyo.
Kama wanaume wangesusa kuoa wanawake waliofanyiwa ukatili huo huenda hali ingebadilika. Tairo anasema, ni vigumu kuwafuatilia watoto wanaopata mimba za utotoni kama hawajaandikishwa shuleni. “Mfano mtoto ni mjamzito na walimu wanamripoti, tunataka maofisa, watendaji wa kijiji na kata wafuatilie yule mhalifu.
Mtoto anapofuatwa anasema alienda kuchota maji akakutana na morani kundi la wanaume au dereva wa lori akambaka. Katika hilo unakuta mzazi sio mkali. Je, wewe wa nje utafanya nini?” Anahoji.
Kwa mujibu wa Tairo, chanzo cha tatizo hilo ni mila, hamasa ndogo kwa elimu hasa kwa watoto wa kike na utajiri wanaoutarajia wazazi kwa kuwa na mtoto wa kike. Anasema, utekelezaji dhaifu wa sera na sheria ngazi ya kijiji kunachangia tatizo hilo liendelee.
Dk Ayubu John (jina si rasmi) anasema watoto wa kike wamekuwa wakifanyiwa ukatili mkubwa kwa kuwa bibi na mama zao hutafuta vibuyu vile vyenye mrija mwembamba kama mrija wa boga, na kuwaingizia kwenye sehemu zake siri.
“Kile kimrija anaingiza kwenye sehemu za siri za mtoto anazungusha taratibu kila siku na njia inaongezeka. Huanza kitendo hicho kwa mtoto taratibu tokea akiwa mdogo hivyo mtoto akifikia miaka 12 mpaka 16 anaweza kuolewa,” anasema daktari huyo.
Anasema hata hizo ndoa za utotoni ni tatizo kubwa kwa sababu watoto wengi wanashindwa kujifungua, pia wengi wanashindwa kuhimili majukumu ya familia na kwamba, hata kunyonyesha hufundishwa.
Mratibu Mtendaji wa Mtandao wa Kuelimisha Jamii kuhusu madhara ya ukeketaji pamoja na aina nyingine za unyanyasaji wa kijinsia (NAFGEN), Francis Selasini anasema, vitu vinavyoharibu elimu ya mtoto wa kike ni ule mtazamo wao kwamba tayari ana mchumba hivyo anakosa morali wa kupenda kusoma.
Daktari huyo anasema, kitendo cha kumlazimisha mtoto aolewe ili wazazi wapate ng’ombe wengi ni ukatili. “Utajiri wa baba mwenye boma ni pale mtoto wake anapokuwa amekeketwa na pia hajapata mimba akiwa nyumbani, wakati wa kumwozesha hupata mali nyingi zaidi,” anasema.
Anashauri Serikali kusaidia taasisi zinazopinga ukatili ili ziweze kufanya kazi vizuri. Kaimu Ofisa Elimu Sekondari, Mwalimu Kamota Kimweri anasema ni vigumu kupata takwimu za ndoa za utotoni kiwilaya.
Anasema mwaka 2013 waliwachukulia hatua wazazi 20 ambao watoto wao walikuwa hawana mahudhurio mazuri shuleni, baada ya hapo tatizo lilipungua. Kimweri anasema, chanzo cha ndoa za utotoni ni mila na mazoea ya Wamasai kuchumbia mimba hivyo mtoto akizaliwa wa kiume huwa rafiki wa mchumbiaji na akizaliwa wa kike huwa ni mke mtarajiwa.
Wamasai wanalipa mahari ya ng’ombe taratibu na ikifika muda mwafaka hudai mke wake. Kimweri anasema elimu ni muhimu kwa watu wanaokubalika katika jamii kama viongozi wa siasa, wa kidini na wa kimila ili wasaidie kubadili mila potofu.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA), kimefanya utafiti katika mikoa 14 ikiwemo mitano ya Zanzibar na kubaini aina tano za ukatili ukiwemo ubakaji, wanafunzi wa shule kulazimishwa kuolewa, ukeketaji, vipigo kwa wanawake pia watoto na wanawake kutelekezwa. Tamwa imefanya utafiti huo kutokana na kushamiri kwa vitendo hivyo, vingi haviripotiwi ama hayapewi vipaumbele inavyostahili katika vyombo vya habari.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
Serikali Yakataa Maombi Yote Ya Shule Binafsi Kupandisha Ada Mwaka Huu
By:
Unknown
On: 23:26
Kamishna
wa Elimu nchini amekataa maombi yote ya shule za msingi na sekondari
zisizo za Serikali kupandisha ada katika mwaka huu wa masomo na ameagiza
shule zilizopandisha ada kinyume cha tamko la Serikali kusitisha ada
hizo mpya.
Kutokana
na uamuzi huo, Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi
imeziagiza shule zote za binafsi ambazo zimepandishia ada kiholela bila
kupata kibali cha wizara hiyo, kurejesha ada waliyokuwa wanatoza mwaka
jana, la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa shule itakayokaidi.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ithibati ya Shule, Hadija Mcheka amesema
baada ya tangazo la wizara hiyo kuzitaka shule binafsi zinazotaka
kupandisha ada kuwasilisha maombi kwa Kamishna wa Elimu na kutoa sababu
za kupandisha ada, ni shule 45 tu zilipeleka maombi ya kupandisha ada
wakati shule zingine 900 ziliomba ziendelee kutoza ada ya mwaka jana.
“Hizi
shule 45 hazikupata kibali cha kupandisha ada maana sababu walizozitoa
hazikumridhisha Kamishna wa Elimu hivyo akaamuru zibakie na ada ya mwaka
jana,” alisema Mcheka.
Tanzania ina jumla ya shule za msingi 14,000 na kati ya hizo shule binafsi ni 1,000.
Tanzania ina jumla ya shule za msingi 14,000 na kati ya hizo shule binafsi ni 1,000.
Kwa
upande wa sekondari, shule binafsi ziko zaidi ya 1,400 kati ya
sekondari 4,000. Mcheka alifafanua kuwa baadhi ya shule zilitoa sababu
kuwa wanapandisha ada kwa sababu wana ujenzi, jambo ambalo kamishna
aliona halimhusu mzazi.
“Mwingine
anasema anataka kupandisha ada kwa vile anataka kuajiri walimu kutoka
nje ya nchi, hili nalo halimhusu mzazi ndio maana tumewanyima kibali cha
kupandisha ada,” alieleza.
Pia
alisema shule zingine zilinyimwa ruhusa ya kupandisha ada kwa sababu
hazikutoa sababu yoyote zaidi ya kueleza kuwa wanataka kupandisha ada
kutokana na gharama za uendeshaji.
“Sababu zote hizi hazikumridhisha kamishna ndio maana tumewataka watii agizo la Serikali hadi hapo baadaye.” Alifafanua.
Mcheka
alisema hatua ya kuzitaka shule zote zibaki na ada ya mwaka jana ni
kutokana na wizara hiyo kumwajiri mtaalamu mwelekezi anayefanya kazi ya
kujua gharama za kumsomesha kila mwanafunzi ili kuisaidia Serikali
kuweka ada elekezi.
Alisema ada elekezi hiyo ndio itakayoisaidia wizara kupanga ada elekezi kwa shule binafsi.
Aliwaonya wamiliki wa shule binafsi ambao wamepuuza agizo hilo kwa kisingizio kuwa hawajapelekewa barua na wizara husika kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria zilizoainishwa wakati shule inaposajiliwa.
Aliwaonya wamiliki wa shule binafsi ambao wamepuuza agizo hilo kwa kisingizio kuwa hawajapelekewa barua na wizara husika kwamba watachukuliwa hatua kali za kisheria zilizoainishwa wakati shule inaposajiliwa.
Alisema
Serikali inafanya kazi kupitia waraka, matamko na maagizo ambayo lazima
wahusika wanaohusika kuyatiii na sio kusubiri kuandikiwa barua.
“Katika
hili hatutanii kama zipo shule ambazo hazikutii tamko lile la Serikali
na wakapandisha ada naomba wasitishe ada hizo mpya,” alionya.
Mcheka
aliwataka wazazi na walezi walioanza kulipa ada hiyo mpya kusitisha
malipo hayo mara moja na kwamba wahakikishe kuwa ada yote watakayolipa
kwa mwaka huu ifanane na ile iliyolipwa mwaka jana na sio vinginevyo.
“Kama
mwaka jana alilipa Sh milioni 1.5 na mwaka huu amepandishiwa hadi Sh
milioni 1.8, na kwa kuwa mzazi analipa kwa term (muhula)na tayari
ameshalipa term ya kwanza, naomba atakapolipa muhula wa pili alipe pesa
pungufu ya kile alicholipa term (muhula) ya kwanza ili zitimie Sh
milioni 1.5 na sio Sh milioni 1.8,” alisema Mcheka.
Aliwataka
wazazi na walezi kutoa taarifa wizarani na ofisi za elimu za wilaya kwa
shule ambazo zitakaidi agizo hilo ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Credit;Mpekuzi blog
Shein: Tuko tayari, shauri yao waliosusa
By:
Unknown
On: 23:24
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akihutubia wanachama wa CCM. |
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amesema chama
hicho kipo tayari kwa uchaguzi wa marudio Machi 20 kwa lengo la
kuhakikisha kinashika dola na waliochukua uamuzi wa kususa ni maamuzi
yao binafsi. Aidha, amesema Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad ndiye aliyekiuka makubaliano ya mazungumzo ya mwafaka na kukimbilia katika vyombo vya habari. Akihutubia mamia ya wanachama wa CCM katika viwanja vya Makao Makuu ya CCM Kisiwandui mjini hapa kuzindua maadhimisho ya miaka 39 ya CCM, Dk Shein alisema maamuzi ya kurudiwa kwa Uchaguzi Mkuu yamefanywa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) ambayo ndiyo chombo halali kwa mujibu wa Katiba cha kushughulikia masuala yote ya uchaguzi nchini. Aliwataka wanachama na wafuasi wao kujipanga vizuri na kushiriki uchaguzi huo kikamilifu kwani kwa mujibu wa Katiba ya CCM ni kushinda uchaguzi zote zinazofanyika nchini ili kushika dola na kuwatumikia wananchi. “Hayo ndiyo maamuzi ya chama chetu tuliyokubaliana kushiriki Uchaguzi Mkuu wa marudio baada ya kufutwa kwa ule wa Oktoba 25 mwaka jana kwa hivyo wanachama na wafuasi jitayarisheni kushiriki kikamilifu kwa ajili ya kushika dola,” alisema Dk Shein. Dk Shein ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alisema amesikitishwa na uamuzi pamoja na kauli za Katibu Mkuu wa CUF ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif za kujitoa katika mazungumzo yaliyokuwa yakifanyika, ambayo wote kwa jumla walikubaliana kwamba yawe siri kwa muda wote. Huku akishangiliwa na wafuasi na wanachama wa CCM, Dk Shein alisema ni Maalim Seif ndiye aliyemuandikia barua kukutana na kufanya mazungumzo kwa ajili ya mustakabali wa wananchi wa Zanzibar, ombi ambalo yeye alikubaliana nalo na kuliwasilisha kwa wenzake na hapo mazungumzo yalianza. Alifahamisha kwamba moja ya masharti ya mazungumzo yao ni kuheshimu na kutunza siri hadi muafaka utakapopatikana kwa kutoa taarifa ya pamoja kwa wananchi, lakini Dk Shein alisema kwa masikitiko makubwa Maalim alishindwa masharti hayo na kujitoa katika mazungumzo. “Nasikitika sana aliyejitoa katika mazungumzo ni mwenzangu Maalim Seif ambaye alikiuka makubaliano yetu na kuamua kwenda mbele ya vyombo vya habari kuzungumza....... mimi ni muungwana bwana naheshimu makubaliano na ndiyo maana nimekaa kimya,” alisema. Aliwataka wananchi na wafuasi wa CCM kujiandaa na uchaguzi wa Machi 20, akitamba kuwa wembe ni ule ule wa kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo na kurudisha na kujenga imani ya wananchi walio wengi ambao anaamini kwamba CCM ndiyo chama kitakacholinda amani na utulivu. Aidha, alisema SMZ haipo tayari kuona kwamba watu wachache wanavuruga amani ya nchi kwa maslahi yao binafsi na uroho wa madaraka na kuwataka wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa marudio Machi 20. “Nasisitiza tena Zanzibar itabakia kuwa na amani katika kipindi cha uchaguzi wa marudio na atakayejaribu kuleta fujo, vyombo vya sheria vitachukua mkondo wake na hakuna sababu ya wananchi kuogopa kwenda kupiga kura kwani suala la uchaguzi wa marudio ni la kawaida ambalo linatokana na matakwa ya kisheria,” alisema. Mapema, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliwataka wanachama na viongozi kwa ujumla kujipanga kuhakikisha kwamba CCM inashinda, akisema uchaguzi ni kujipanga na kuweka mikakati pamoja na mahesabu. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatimiza miaka 39 tangu kilipozaliwa Februari 5, 1977 baada ya kuvunjwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa kwa chama hicho kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano na mapenzi ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kilele cha sherehe kitakuwa mjini Singida Jumamosi wiki hii. Chanzo Gazeti la habariLeo. |
Mabenki yatiwa kitanzini
By:
Unknown
On: 23:20
Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango. |
SERIKALI imeanza kuchukua hatua za kupunguza riba za mabenki kwa wananchi kwa kuagiza akaunti za mashirika na taasisi zake katika mabenki ya biashara zifungwe na kuhamisha fedha zilizoko katika akaunti hizo kwenda akaunti zitakazofunguliwa Benki Kuu (BoT).
Agizo hilo limetolewa na Msajili wa Hazina, Lawrence Mafuru hivi karibuni, akiwataka watendaji wakuu wote wa mashirika na taasisi hizo, kufuata maelekezo matano ya kufunga akaunti zao katika mabenki ya biashara na kuhamishia fedha hizo BoT.
Katika agizo la kwanza watendaji hao, wametakiwa kufungua akaunti ya mapato yao kwa aina ya fedha za mapato wanayopokea, kama ni za kigeni au Shilingi za Tanzania, katika tawi la karibu yao la BoT haraka iwezekanavyo kabla ya jana.
Baada ya kufungua akaunti hizo, watendaji hao wametakiwa kuelekeza makusanyo yote ya fedha za ofisi zao ikiwemo fedha za ruzuku zinazotoka serikalini kwenda katika akaunti mpya zilizofunguliwa katika matawi ya BoT.
Agizo la tatu la Serikali kwa watendaji hao wametakiwa kuhamisha fedha zote zilizobakia katika akaunti zao zilizoko katika mabenki hayo ya biashara na kupeleka katika akaunti mpya zilizoko BoT.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uhusiano pekee kati ya mashirika hayo na mabenki ya biashara itakuwa akaunti itakayohifadhi fedha za uendeshaji ambayo imetakiwa kuwa na fedha zinazotosha uendeshaji wa shughuli za taasisi zao kwa mujibu wa matarajio ya matumizi yao ya kila mwezi.
Hata hivyo, katika agizo la tano watendaji hao wameaswa kuhakikisha fedha yoyote itakayokuwepo katika akaunti hizo kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za taasisi, ihakikishwe inapata mapato ya riba kulingana na viwango vya riba vilivyopo katika soko.
Utekelezaji Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu kuhusu utekelezaji, Mafuru alisema tayari baadhi ya mashirika na taasisi hizo zimeshatoa taarifa za utekelezaji wa maagizo hayo.
Alifafanua kwamba si rahisi kwa mashirika yote kufanikisha hatua zote ndani ya muda waliopewa unaokwisha leo, kwa kuwa baadhi ya mashirika, ufunguzi wa akaunti ni lazima ufanyike kwa uamuzi wa bodi ya wakurugenzi.
Mafuru alisema akaunti zingine za mashirika na taasisi hizo, ziko katika akaunti za muda maalumu katika benki hizo za biashara, hivyo kabla ya kuzifunga na kuhamisha fedha husika, kutahitajika majadiliano kati ya shirika au taasisi husika na benki yake.
Kwa mujibu wa Mafuru, la muhimu ni kuanza utekelezaji wa agizo hilo na tayari taasisi hizo, zimeshatoa taarifa ya utekelezaji wake. Sababu Akizungumzia sababu ya hatua hiyo, Mafuru alisema fedha za mashirika na taasisi hizo ni za Serikali na baadhi ya mashirika ambayo hutumia fedha za ruzuku ya Serikali pia huweka fedha hizo katika mabenki hayo.
Akifafanua alisema wakati mwingine mashirika hayo hupelekewa fedha za ruzuku nyingi kuliko mahitaji yao ya wakati huo na Serikali ikipungukiwa na kutafuta fedha za kukopa kutoka vyanzo vya ndani, mabenki hayo huchukua fedha hizo za ruzuku na kuzikopesha kwa Serikali kupitia mnada wa hati fungani za Serikali.
Kwa mujibu wa Mafuru, katika mazingira hayo Serikali hujikuta ikikopeshwa fedha zake yenyewe na wakati wa kulipa mikopo hiyo, hulazimika kulipa na riba ambayo ni fedha ya wananchi inayotumika kulipa mabenki hayo, wakati ingeweza kufanya kazi zingine za maendeleo ya wananchi.
Kushuka kwa riba Kuhusu athari ya hatua hiyo kwa uchumi na hasa katika mzunguko wa fedha, Mafuru alisema kumekuwa na mtazamo ambao si sahihi, kwamba mzunguko wa fedha utapungua.
Alisema wenye mtazamo huo wanasahau kwamba BoT ni benki na mabenki yanapopungukiwa fedha, hukopeshana yenyewe kwa yenyewe na kutozana riba, lakini pia yana fursa ya kwenda kukopa BoT.
Kwa mujibu wa Mafuru, kwa kuwa BoT kwa hatua hiyo itakuwa na fedha nyingi, mbali na kuikopesha Serikali wakati itakapopungukiwa fedha, lakini pia itakopesha mabenki ya biashara pale yatakapopungukiwa fedha.
Katika hatua hiyo, alisema BoT itakopesha mabenki ya biashara kwa riba ndogo kuliko inayotumika na mabenki hayo wakati wa kukopeshana yenyewe kwa yenyewe, hivyo kutumia fursa hiyo kudhibiti riba ya mabenki hayo kwa mikopo itakayotolewa kwa wananchi.
Alisema hatua hiyo ni rahisi kwa BoT kuongeza mzunguko wa fedha, kwa kuwa na yenyewe itakuwa ikikopesha mabenki hayo kwa riba ndogo, ili mabenki hayo ya biashara yakopeshe wananchi kwa riba ndogo, hivyo kuyadhibiti kibiashara kuliko kushinikiza mabenki kupunguza riba, wakati yapo katika soko la ushindani.
Matakwa ya Magufuli Itakumbukwa Rais Magufuli alipokutana na wafanyabiashara mwishoni mwa mwaka jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alisema anafahamu Tanzania ina benki kubwa karibu 54 na zote zinafanya biashara na Serikali, lakini zote hizi hazijajikita chini kwenda kwa wananchi.
Dk Magufuli alisema alijaribu kufanya uchambuzi akakuta karibu Sh bilioni 550 zinazozunguka katika benki hizo, ni fedha za umma ambazo kiukweli ni fedha za Serikali na hivyo Serikali inapouzia benki hizo hati fungani na kuzilipa na riba, inajikuta ikifanya biashara na mabenki hayo kwa kutumia fedha zake yenyewe.
Siku hiyo Dk Magufuli alisema mabenki haya ndiyo katika hesabu zao wanaonesha wana hifadhi kubwa ya fedha wakimaanisha kwamba wanazo fedha zimewekwa ambazo ni visenti vya Watanzania, lakini Watanzania wenyewe hawakopesheki, hawapati mikopo na kuhoji fedha hizo zinakopelekwa.
Kauli ya Dk Mpango Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango siku ya kuapishwa kushika wadhifa huo, aliahidi kushughulikia tatizo la riba kubwa inayotolewa kwenye benki nchini jambo linalochangia kushusha idadi ya watu wanaokwenda benki kukopa.
Alisema lazima sekta ya fedha isimamiwe vizuri ili kila mwananchi akope na kueleza dhamira yake kuwa atahakikisha riba za mikopo zinashuka ili wananchi wajipatie mikopo kwa riba nafuu.
Kwa sasa riba za mikopo katika benki mbalimbali zimekuwa kubwa zinazofikia asilimia 21, jambo ambalo limekuwa likihojiwa na wataalamu mbalimbali, kwani mfumuko wa bei ambao ndio wenye kawaida ya kusababisha gharama za mkopo kuwa juu, upo chini ya asilimia 10 kwa muda mrefu sasa.
Aidha, kumekuwepo tofauti kubwa kati ya riba ya kuweka fedha na riba ya kukopa fedha kwani mwananchi akiweka fedha zake benki, amekuwa akilipwa riba ndogo ya asilimia tatu wakati akienda kukopa fedha anatozwa riba ya asilimia mpaka 21.
Kutokana na hali hiyo, pamoja na kuwepo kwa taasisi nyingi za benki, wafanyabiashara wamekuwa wakilalamika kuwa mfumo wa fedha umekuwa ukishindwa kukusanya akiba kwa wingi na kuiwekeza kwa wajasiriamali wa ndani ili kukuza uchumi na kuongeza ajira.
Aidha, wataalamu wengi wamekuwa wakionya kwamba biashara inayofanyika kati ya mabenki na Serikali, kwa mabenki hayo kukopesha Serikali kwa kununua Hati Fungani za BoT na kurejeshewa fedha zao kwa riba kubwa, imekuwa ikiwapa mabenki hayo faida kubwa na kusababisha yaache kufanya biashara na wananchi wanaokopa fedha kidogo na hivyo kuwapandishia wananchi riba.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
Mahakama Yashusha Rungu kwa Majangili........Yawapiga Kifungo cha Miaka 20 na Faini ya Milioni 270
By:
Unknown
On: 23:16
Mahakama
ya Wilaya ya Manyoni, mkoani Singida, imewahukumu mtu na kaka yake,
kutumikia kifungu cha miaka 20 kila mmoja na kulipa fidia ya sh. milioni
270, baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya kukutwa na meno ya tembo,
silaha na risasi kinyume cha sheria.
Washitakiwa
hao ni Nicodem Mchongareli na Festol Mchongareli, ambao walikuwa
wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 13 ya mwaka jana.
Wanadaiwa
kukutwa na meno ya tembo mawili yenye thamani ya sh. milioni 27,
bunduki tatu zikiwemo za aina ya Riffle, risasi 25 na maganda yake 15.
Hukumu
hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Joyce Minde, baada ya upande wa Jamhuri
uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Salim Msemo na ule wa utetezi
kufunga ushahidi.
Akisoma
hukumu hiyo, Hakimu Joyce alisema wakati wa usikilizwaji wa shauri
hilo, upande wa jamhuri ulileta mashahidi watano na washitakiwa baada ya
kuonekana wana kesi ya kujibu walijitetea wenyewe.
“Mahakama
imewaona washitakiwa hao wana hatia baada ya upande wa Jamhuri
kuthibitisha mashitaka dhidi yao pasi na kuacha shaka yoyote,” alisema.
Hakimu
huyo aliwapa adhabu washitakiwa hao kwa kukutwa na meno ya tembo,
kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja na kulipa serikali sh.
milioni 270.
Pia
shitaka la pili wamehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka miwili jela au
kulipa faini ya sh. milioni 333 na makosa mengine kutumilia kifungo cha
miaka miwili au kulipa faini ya sh. milioni mbili kwa kila shitaka.
Adhabu za vifungo zinakwenda sambamba, hivyo washitakiwa hao watatumikia kifungo cha miaka 20 kila mmoja
Credit; Mpekuzi blog
Ligi kuu England kuendelea Jumanne
By:
Unknown
On: 23:14
Ligi kuu ya England
inatarajia kuendelea tena jumanne kufuatia mapumziko ya michuano ya FA,
kwa michezo kadhaa,ambapo Arsenal watawakaribisha Southampton,Leicester
city watakuwa wenyeji wa Liverpool, Norwich watakuwa wakimenyana na
Tottenham Hotspurs.
Michezo mingine Sunderland watawaalika
Manchester City, Aston Villa watakuwa wageni wa West Ham United,Crystal
Palace watawakaribisha Bournemouth, Stoke watakuwa wenyeji wa Manchester
Unted na West Brom watachuana na Swansea city.Mpaka sasa Leicester city wanaongoza ligi kwa alama 47 ikifuatiwa na Manchester city katika nafasi ya pili,nafasi ya tatu ni Arsenal na nafasi ya nne ni Tottenham.
Chanzo BBC Swahili.
Askofu Mpya KKKT Aonya Utumbuaji MAJIPU.......Amtahadharisha Rais Kutumbua Majipu kwa Haki, Asema Bunge Halipaswi Kulindwa na Jeshi
By:
Unknown
On: 23:08
***
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick
Shoo ameitahadharisha Serikali kuhusu zoezi la Utumbuaji Majipu
linaloendelea akiitaka kuzingatia misingi ya haki na busara ya Ki-mungu
ili kutowapa nafasi watu wasio waaminifu kuitumia vibaya kufanya
ukandamizaji.
Askofu
Shoo aliyasema hayo jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro, katika ibada
maalum ya kuingizwa kazini iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Alisema
kuwa Kanisa lina imani na Serikali ya Awamu ya Tano na kupongeza juhudi
zake katika kupambana na watumishi wa wanaojihusisha na ubadhirifu wa
mali za umma pamoja na mafisadi, lakini zoezi la kutumbua majipu
linapaswa kuchukuliwa kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka uonevu.
“Utumbuaji
huu ufanyike katika misingi ya haki na kwa busara kwani watu wengine
wanaweza kutumia mwanya huu kuonea wenzao wasiokuwa na hatia,” alisema Askofu Shoo.
Katika
hatua nyingine, Askofu Shayo alielezwa kusikitishwa na vitendo vya
utovu wa nidhamu vinavyofanywa na baadhi ya wabunge wanapokuwa Bungeni.
“Tunahitaji
kuona Bunge linajadili vikao vyake kwa uwazi na kwa kuzingatia misingi
ya demokrasia. Kanisa linasikitishwa sana na vitendo vya utovu wa
nidhamu vinavyoendelea bungeni. Tunapenda kuona hoja zinajadiliwa kwa
ustaarabu,” alieleza.
Kadhalika,
Askofu Shayo aliionya matumizi ya jeshi la Polisi ndani ya Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa Bunge ni sehemu ya
Demokrasia na kamwe haipaswi kulindwa na jeshi. Aliongeza kuwa Bunge
linapaswa kuendeshwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia na uwazi.
Aliihakikishia
serikali kuwa Kanisa litaendelea kuunga mkono juhudi za maendeleo ikiwa
ni pamoja ikiwemo sekta ya elimu na afya. Aliishauri Serikali kuangalia
upya sera ya elimu bure na kuboresha utoaji wa elimu hiyo.
Naye
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alizishukuru taasisi za dini kwa
kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo kupitia sekta
mbalimbali na kuzihimiza kuendelea kuwekeza katika maeneo muhimu
yakiwemo ya Afya na elimu.
“Napenda
kutumia fursa hii kuyashukuru madhehebu ya dini ambayo yamekuwa mstari
wa mbele kusaidia Serikali katika kufikisha huduma hizi za afya karibu
zaidi na wananch. Wito wangu kwa hili, naombeni mjitahidi kutoa huduma
hizi kwa gharama nafuu ili wananchi wengi waweze kuzitumia,” Waziri Mkuu Majaliwa ananukuliwa.
Ibada hiyo maalum ilihudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.
Credit; Mpekuzi blog
Magufuli alaani kuuawa kwa rubani porini
By:
Unknown
On: 23:06
Rais wa Tanzania
John Magufuli amesema amesikitishwa sana kitendo cha kuuawa kwa rubani
Mwingereza aliyekuwa akisaidiana na maafisa wa Tanzania kupambana na
ujangili.
Rubani wa helkopta Kapteni Roger Gower, alifariki baada
ya majangili kuifyatulia risasi na kuidondosha helkopta aliyokuwa
akiiendesha wakati alipoungana na askari wanyamapori waliokuwa
wakikabiliana na majangili katika pori la akiba lililopo katika wilaya
ya Meatu Mkoani Simiyu.Askari mmoja wa Tanzania alijeruhiwa wakati wa kisa hicho.
Tembo watatu pia walipatikana wakiwa wameuawa.
Dkt Magufuli ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha waliomuua rubani huyo wanakamatwa na wanafikishwa mikononi mwa vyombo vya sheria, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa kurugenzi ya mawasiliano ya ikulu.
Polisi tayari wamewakamata washukiwa watatu kuhusiana na mauaji hayo.
Kiongozi huyo amesema serikali yake itahakikisha inaendeleza mapambano dhidi ya ujangili kwa nguvu zake zote.
Amewataka wananchi na wadau mbalimbali wa hifadhi ya wanyamapori, kutokatishwa tamaa na tukio hilo na wasaidie kuwafichua watu wote wanaojihusisha na ujangili ama biashara ya bidhaa zitokanazo na ujangili.
Hivi karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.
Uwindaji haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji haramu.
Chanzo BBC Swahili.
UKAWA Wapinduliwa....Kamati Iliyoibua Sakata la Escrow Yakabidhiwa Kwa Wabunge wa CCM
By:
Unknown
On: 23:02
Wabunge wa upinzani, wakiwamo wanaootoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamepata pigo la aina yake baada ya jukumu mojawapo muhimu la kamati wanayopaswa kuiongoza kuondolewa kwao, imefahamika.
Kamati
hiyo ni ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) ambayo
imehamishiwa kwenye kamati mpya inayoongozwa na wabunge wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM).
Majukumu hayo muhimu yaliyohamishwa PAC ni yale yanayohusiana na hesabu za mashirika ya umma.
Majukumu
hayo sasa yamehamishiwa kwenye kamati mpya ya Bunge ya Uwekezaji na
Mitaji ya Umma (PIC), chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Jimbo la Sumve
(CCM), Richard Ndasa, huku makamu mwenyekiti akiwa Lolesia Bukwimba
(Busanda-CCM).
Naibu
Katibu wa Bunge anayeshughulikia masuala ya Bunge, John Joel,
amethibitisha juu ya kuwapo kwa mabadiliko hayo, akisema kwamba ni
kweli PIC imepewa jukumu la kusimamia hesabu za mashirika ya umma
kutokana na kanuni za Bunge, toleo la Januari 2016.
Alisema uamuzi wa kupeleka jukumu hilo PIC, umetokana na pendekezo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kutokana na PAC iliyopita kushindwa kutimiza majukumu yake iliyopewa.
Katika
mabunge yaliyotangulia, hesabu za mashirika ya umma zilikuwa
zikisimamiwa na Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), iliyokuwa ikiongozwa
na Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia (Chadema), Zitto Kabwe. Hivi
sasa, Zitto ni Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo.
Kamati hiyo pia iliwahi kuongozwa na aliyekuwa Mbunge wa Bariadi Mashariki (UDP), John Cheyo.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa mara zote PAC ndiyo iliyokuwa mstari wa mbele katika
kuibua ‘madudu’ mbalimbali yanayohusiana na rushwa na ufisadi bungeni na
kuilazimu serikali kubadili mawaziri wake mara kadhaa.
Baadhi
ya mambo yaliyowahi kuibuliwa na PAC ni pamoja na kashfa ya Akaunti ya
Tegeta Escrow ambayo ripoti yake ilisababisha mawaziri wawili wa
serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete na maofisa wengine
kadhaa wa juu kuachia ngazi.
Taarifa ya PAC kuhusiana na ripoti ya CAG mwaka 2012 pia ilisababisha vigogo kadhaa, wakiwamo mawaziri, kung’olewa.
Taarifa ya PAC kuhusiana na ripoti ya CAG mwaka 2012 pia ilisababisha vigogo kadhaa, wakiwamo mawaziri, kung’olewa.
Zitto Atoa ufafanuzi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa PAC kwenye Bunge la 10, Zitto, amesema si kweli kwamba kuna jukumu walilopewa na kushindwa kulitimiza.
“Kwa
kweli tulitimiza majukumu yetu yote. Na ili tufanye kazi yetu kwa
ufanisi, tuliigawa kamati, eneo moja likawa chini ya Makamu Mwenyekiti
(Deo Filikunjombe) na moja chini yangu. Deo mashirika na mimi serikali.
"Hata
hivyo, kazi ilikuwa kubwa na muhimu kugawa PAC kuwa na PIAC na PAC.
Isipokuwa, PIC ya sasa haina mamlaka ya kushughulikia hesabu za
mashirika ya umma kwa mujibu wa kanuni. Kamati za mahesabu ni mbili tu,
PAC na LAAC,” alisema Zitto.
Aliongeza
kuwa iwapo Bunge linataka PIC ishughulike na hesabu za mashirika ya
umma, itabidi iitwe Public Investments Account Committee (PIAC) na
itabidi iongozwe na mbunge wa upinzani na siyo wa CCM.
“Kanuni
za Bunge za sasa hazielekezi PIC kushughulikia taarifa ya CAG kuhusu
mahesabu ya mashirika ya umma. Pia kanuni haziipi PAC mamlaka hayo pia.
Kikanuni, hivi sasa mahesabu ya mashirika ya umma hayana kamati,” alisema Zitto.
Credit;Mpekuzi blog
Meli kubwa iliyoinama yazua wasiwasi Ufaransa
By:
Unknown
On: 22:56
Meli ya kubwa
iliyoegemea upande mmoja inakaribia kufika katika pwani ya Ufaransa,
maafisa wa bahari wanasema, ingawa kuna matumaini ya kuiokoa kabla ya
kuzama.
Meli hiyo kwa jina Modern Express ambayo, imesajiliwa
Panama, ilianza kulala upande mmoja Jumanne baada ya kutokea kwa
hitilafu za kimitambo.Mabaharia wote 22 wameondolewa kutoka kwenye meli hiyo.
Juhudi za kuisimamisha zimefeli, lakini maafisa wanasema jaribio jingine litafanywa leo Jumatatu.
Juhudi za leo zikishindikana, basi meli hiyo itagonga pwani ya Ufaransa kati ya Jumatatu usiku na Jumanne asubuhi.
Hali mbaya ya hewa ilitatiza juhudi za uokoaji Jumapili.
Meli hiyo imebeba tani 3,600 za mbao na mashine kadha za uchimbaji, na imeinama kwa pembe ya kati ya nyuzi 40 na 50.
Ina tani 33 za mafuta.
Mwaka 2002, meli ya kusafirisha mafuta kwa jina Prestige ilizama karibu na pwani ya Uhispania na kumwaga mafuta tani 50,000 na kuchafua eneo kubwa la bahari.
Chanzo BBC Swahili.
Nigeria yaomba mkopo wa dharura
By:
Unknown
On: 22:43
Nigeria inaomba
mkopo wa dharura wa jumla ya dola bilioni tatu unusu kutoka kwa Benki ya
Dunia kujaribu kuziba pengo kwenye bajeti yake.
Uchumi wa Nigeria umeathiriwa sana na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.Waziri wa fedha nchini humo Kemi Adeosun amesema amekuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Benki ya Dunia.
Hatua ya Nigeria kuomba mkopo wa dharura inashangaza ikizingatiwa kwamba siku chache zilizopita Shirika la Fedha Duniani (IMF) lilisema haihitaji usaidizi wa kifedha.
Serikali mpya ya Rais Muhammadu Buhari ilikuwa imeacha pengo katika ufadhili wa bajeti yake katika juhudi za kujaribu kusisimua uchumi wa taifa.
Lakini tofauti kati ya mapato na matumizi imeendelea kuongezeka na kuilazimu Nigeria kuomba usaidizi kutoka nje.
Nigeria silo taifa la pekee kuathiriwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
Azerbaijan, nchi nyingine inayozalisha mafuta kwa wingi, pia imeanza mazungumzo na Benki ya Dunia.
Uchumi wa Venezuela nao umekuwa katika hali ya tahadhari.
Kushuka kwa bei ya mafuta kulichangia sana katika kushuka kwa jumla ya mapato ya taifa Urusi mwaka jana.
Chanzo BBC Swahili.
Diamond Platnumz Kazinyakua Tuzo Nyingine Kubwa Usiku wa Jana.
By:
Unknown
On: 06:58
Mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz amezidi kuziandika headline katika ulimwengu wa
sanaa baada ya usiku wa leo kuzinyakua tuzo mbili za Hipipo Awards zilizofanyika Uganda.
Ushindi alioupata ni Nyimbo bora Afrika Mashariki na Video bora Afrika Mashariki ambazo zote ni kupitia wimbo wa Nana.
Baada ya ushindi kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika maneno haya
“Wow! Realy wanna Thank GOD for keep blessing the innocent kid… also wana thank all Media and My Loyal fans for the Big love.. Two Awards tonight on @HipipoAwardsUGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT#NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO#NANA many thanks to my brother@2niteflavour
@i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent!
(Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI#NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechkua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana“.
Millard Ayo.com
sanaa baada ya usiku wa leo kuzinyakua tuzo mbili za Hipipo Awards zilizofanyika Uganda.
Ushindi alioupata ni Nyimbo bora Afrika Mashariki na Video bora Afrika Mashariki ambazo zote ni kupitia wimbo wa Nana.
Baada ya ushindi kupitia account yake ya Instagram Diamond aliandika maneno haya
“Wow! Realy wanna Thank GOD for keep blessing the innocent kid… also wana thank all Media and My Loyal fans for the Big love.. Two Awards tonight on @HipipoAwardsUGANDA…EAST AFRICA SUPER HIT#NANA and EAST AFRICA BEST VIDEO#NANA many thanks to my brother@2niteflavour
@i_am_godfather and all Behind this Hit!!!… thanks alot @HIPIPOAwards for keep supporting the real African talent!
(Wadau kijana wenu nimefanikiwa kushinda tunzo mbili Usiku wa leo kama NYIMBO BORA AFRICA MASHARIKI#NANA na VIDEO BORA AFRICA MASHARIKI #NANA nawashkuru sana kwa kura na support zote mnazoendelea kunipa….. tafadhali nisaidieni kuhesabu ni tunzo ngapi tumechkua tangu Mwaka 2016 uanze? ) shukran sana“.
Millard Ayo.com
Apendekeza wakimbizi wapigwe risasi Ujerumani
By:
Unknown
On: 06:15
Mwanasiasa mmoja
mbishi nchini Ujerumani ameibua hasira kubwa, baada ya kupendekeza kuwa
maafisa wa polisi wanafaa kuruhusiwa kuwapiga risasi wahamiaji,
wanaojaribu kuingia nchini humo bila idhini.
Kiongozi mkuu wa
chama cha mrengo wa kulia cha Alternative for Germany Frauke Petry,
ameliambia gazeti la Mannheimer Morgen, kwamba anapendekeza matumizi ya
silaha kwa polisi kama hatua ya mwisho.Sheria za polisi wa Ujerumani zinasema kuwa hakuna sheria inayodhinisha kushambulia wakimbizi kwa risasi.
Mwanachama mmoja mkuu wa chama cha Social Democrats, amemkumbusha Frauke Petry kwamba, mwanasiasa wa mwisho wa iliyokuwa Ujerumani mashariki, ambaye alimuru wakimbizi kupigwa risasi, alikuwa Erich Honecker, kiongozi mkuu wa utawala wa kikomunisti ambao ulisambaratika mwaka 1989.
Chanzo BBC Swahili.
Wawindaji haramu wamuua rubani nchini Tz
By:
Unknown
On: 06:12
Shirika moja la
wakfu wa utunzaji wa mazingira, linasema kuwa rubani mmoja raia wa
Uingereza, amepigwa risasi na kuuawa nchini Tanzania.
Rubani huyo anasemekana kuwa alikuwa akipepeleza mzoga wa ndovu porini alipodunguliwa na mwindaji haramu aliyekuwa amejificha .Operesheni hiyo ilikuwa katika mbuga ya wanyama pori ya Maswa Kaskazini mwa Tanzania.
Shirika hilo lenye makao yake nchini Marekani- The Friedkin Conservation Fund, linasema kuwa rubani Roger Gower, alikuwa akiwasaidia utawala nchini Tanzania kukabiliana na wawindaji haramu katika maeneo ya Serengeti, aliposhambulia .
Maafisa wakuu wa serikali ya Tanzania, wanasema kwamba bwana Gower alifaulu kutua helikopta hiyo lakini akafariki muda mfupi baadaye kutokana na majeraha ya risasi.
Hadi sasa hakuna aliyekamatwa kwa mauaji hayo.
Inaaminika kuwa mvamizi alikuwa na bunduki yenye uwezo mkubwa kwani iliweza kupenya ubavu wa ndege hiyo na kumjeruhi marehemu.
Familia ya marehemu inatarajiwa nchini Tanzania hii leo kuandaa mipango ya maziko.
Hivi karibuni, utawala nchini Tanzania umekuwa ukikosolewa kwa kushindwa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na uwindaji haramu wa pembe za ndovu.
Uwindaji haramu umeenea sana katika pori ya Maswa na sio tukio la kwanza ambapo wanaharakati wanaolinda wanyama wa porini wanashambuliwa na wawindaji haramu.
Chanzo BBC Swahili.
Alshabab wavamia tena eneo la Mpeketoni Kenya
By:
Unknown
On: 06:08
Watu wanne wameripotiwa kuuawa katika eneo la Bondeni Mpeketoni katika jimbo la Lamu.
Waliotekeleza shambulizi hilo wanadaiwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabab ambao walikuwa wamevalia magwanda ya kijeshi.Walioshuhudia shambulizi hilo wanasema kuwa wapiganaji wao waliwaruhusu waislamu kuondoka huku wale waliokuwa wakristo wakishambuliwa kwa visu na wengine kwa risasi .
Wenyeji wanasema kuwa shambulizi hilo lilitokea mwendo wa saa kumi alfajiri.
Watu wengi waliachwa wakiuguza majeraha.
Nyumba kadha za wenyeji ambao sio waislamu zilichomwa moto.
Operesheni ya uokozi inayoendeshwa na maafisa wa usalama inaendelea katika eneo lililoko karibu na msitu wa Boni ambako inadaiwa wavamizi hao walitorokea.
Hii si mara ya kwanza kwa eneo hilo la Mpeketoni kushambuliwa na wanamgambo wa Al Shabab.
Mwaka 2014 wanamgambo wa Al shabab walishambulia mji wa Mpeketoni na kuua zaidi ta watu 60.
Washukiwa wakuu wa shambulizi hilo la kwanza Mpeketoni walifikishwa mahakamani majuzi na kusomewa mashtaka dhidi yao.
Chanzo BBC Swahili.
Marais wapinga kutuma jeshi la AU Burundi
By:
Unknown
On: 06:01
Muungano wa Afrika AU hautatuma kikosi cha walinda amani hadi pale serikali ya rais Pierre Nkurunziza itakapotoa mwaliko.
Msemaji
wa Muungano wa Afrika AU, amesema kuwa umoja huo hautatuma majeshi ya
kulinda amani nchini humo hadi pale watakapopokea mwaliko kutoka kwa
taifa hilo la kanda ya Afrika Mashariki.Kauli hiyo ni kinyume na pendekezo la awali la umoja huo ambao uliibua taharuki kuhusu uhalali wake na wajibu wake wa kulinda maisha ya wananchi.
Mjumbe maalum wa umoja huo kanda ya maziwa makuu Ibrahima Fall, anasema kuwa haijawahi kuwa nia ya AU kutuma walinda amani, bila ya idhini ya taifa husika.
-
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, aliwaambia viongozi wa Afrika kwamba anaunga mkono pendekezo lao la kutuma askari 5,000 wa kuweka amani huko Burundi.
Mkutano wa viongozi na marais wa Afrika huko
Ethiopia ulishindwa kupitisha mswada uliohitajika ilikuwatuma wanajeshi
wapatao 5000 kulinda amani nchini Burundi kufuatia mauaji ya mamia ya
wapinzani wa rais Nkurunziza.
Machafuko nchini humo yalitibuka baada ya Nkurunziza kutangaza nia ya kuwania uchaguzi katika muhula wake wa tatu.
Wapinzani wake walisema Nkurunziza alikuwa anakiuka katiba ya taifa na kisha maandamano yakaanza kukotokea hata jaribio la mapinduzi ambayo ilizimwa na kisha rais huyo akaibuka mshindi katika uchaguzi ambao ulisusiwa na baadhi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani.
Kulikuwa na pendekezo la kutuma kikosi cha wapiganaji 5,000 wa muungano wa Afrika ilikuokoa maisha ya wapinzani wa rais huyo.
Awali rais Nkurunziza alionya kuwa majeshi yake yangewakabili vikali jeshi hilo ''Vamizi'' akisema kuwa nchi hiyo iko salama na kuwa ni vitongoji vichache tu vya Bujumbura ambavyo ni ngome ya upinzanani.
Kauli ya mwaka jana wa Nkurunziza kuamua kuwania urais kwa muhula wa tatu ilisababisha vurugu nchini humo, ambapo mamia ya watu wameuwawa na wengine wengi wakitorokea mataifa jirani.
Chanzo BBC Swahili.
Thursday, 28 January 2016
Joseph Fiennes amuigiza Michael Jackson
By:
Unknown
On: 22:40
Muigizaji wa filamu
kutoka nchini Uingereza Joseph Fiennes, amekiri kuwa alishangazwa na
kitendo cha kumuigiza mfalme wa muziki aina ya POP, Michael Jackson
katika mchezo wa runinga ,baada ya kukosekana kwa muigizaji mweupe.
Muigizaji
huyu atakayeigiza kama mwanamuziki katika vichekesho vinavyorushwa na
mtandao wa ''sky network" unaohusu safari ya barabarani iliyofanywa na
Michael Jackson na marafiki zake kina Marlon,Brando na Elizabeth Taylor
baada ya uvamizi wa mara 9-11.Fiennes alieleza kuwa tabaka hilo la kati halikuwa chaguo lake lakini alisema Michael Jackson alikuwa na tatizo la rangi yake ngozi kutokuwa ya asili,hivyo suala la utofauti wa rangi halikuwa kikwazo kwake .
Chanzo BBC Swahili.
Pacha wa Kanumba Adaiwa Kuwa Mhamiaji Haramu
By:
Unknown
On: 22:31
Mkali wa filamu Bongo, Rammy Gallis ‘Pacha wa Kanumba ’ anadaiwa kuishi
nchini bila vibali maalum, jambo linalomuweka hatarini muda wowote
kuweza kutimuliwa Bongo kutokana na tumbuatumbua ya Serikali ya Rais
John Pombe Magufuli inayoendelea.
Kwa mujibu wa chanzo, kuna hatihati kubwa ya msanii huyo ambaye wengi wamezoea kumuita Msomalia kufungashiwa virago kwani hana uhalali wa kuendelea kuwepo nchini.
“Yaani kwa hii kasi ya Mh. Magufuli sidhani kama Rammy atasalimika, si unaona jinsi ambavyo mzee wa kutumbua majipu yupo makini kwenye uongozi wake, yule kaka ni mkimbizi yaani akae tayari kwa safari ya kurudi kwao huko,” kilisema chanzo.
Baada ya kupata madai hayo, Showbiz Xtra ilimpo-vutia waya msanii huyo ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo alijibu;
“Mimi ni Mtanzania halali nina vigezo vya kuwepo Bongo, mama yangu ni Msomali baba ni Muarabu kachanganya na Mbrazil.”
Chanzo: GPL
Kwa mujibu wa chanzo, kuna hatihati kubwa ya msanii huyo ambaye wengi wamezoea kumuita Msomalia kufungashiwa virago kwani hana uhalali wa kuendelea kuwepo nchini.
“Yaani kwa hii kasi ya Mh. Magufuli sidhani kama Rammy atasalimika, si unaona jinsi ambavyo mzee wa kutumbua majipu yupo makini kwenye uongozi wake, yule kaka ni mkimbizi yaani akae tayari kwa safari ya kurudi kwao huko,” kilisema chanzo.
Baada ya kupata madai hayo, Showbiz Xtra ilimpo-vutia waya msanii huyo ili kusikia kauli yake kufuatia madai hayo alijibu;
“Mimi ni Mtanzania halali nina vigezo vya kuwepo Bongo, mama yangu ni Msomali baba ni Muarabu kachanganya na Mbrazil.”
Chanzo: GPL
Diamond Atamani Nafasi ya Waziri Nape title
By:
Unknown
On: 22:28
MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ (Diamond
Platinum), amesema pindi atakapoacha muziki atatumikia siasa huku
akitamani kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Msanii huyo aliweka wazi mpango wake huo hivi karibuni alipohojiwa katika kipindi cha Papaso kinachoongozwa na mtangazaji, Di’jaro Arungu ambapo aliweka wazi kwamba akiingia katika siasa atalenga kuwa Waziri wa Michezo pindi Waziri Nape Nnauye atakapomaliza muda wake.
“Kwa hivi sasa bado sijaingia kwenye siasa ila nikiingia baadaye atakapomaliza Nape nafasi yake nitachukua mimi,’’ alieleza na kuongeza:
“Kile cheo nakiweza kwa sababu mambo ya mpira, movie nayaweza na nikiwa waziri nitavifanya viweze kuleta maendeleo makubwa,” alieleza bila kufafanua atabadilishaje viwe vya maendeleo tofauti na wanavyofanya viongozi wa sasa.
Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani na mwaka gani.
Chanzo Mtanzania
Msanii huyo aliweka wazi mpango wake huo hivi karibuni alipohojiwa katika kipindi cha Papaso kinachoongozwa na mtangazaji, Di’jaro Arungu ambapo aliweka wazi kwamba akiingia katika siasa atalenga kuwa Waziri wa Michezo pindi Waziri Nape Nnauye atakapomaliza muda wake.
“Kwa hivi sasa bado sijaingia kwenye siasa ila nikiingia baadaye atakapomaliza Nape nafasi yake nitachukua mimi,’’ alieleza na kuongeza:
“Kile cheo nakiweza kwa sababu mambo ya mpira, movie nayaweza na nikiwa waziri nitavifanya viweze kuleta maendeleo makubwa,” alieleza bila kufafanua atabadilishaje viwe vya maendeleo tofauti na wanavyofanya viongozi wa sasa.
Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba ataingia kwenye siasa kupitia chama gani na mwaka gani.
Chanzo Mtanzania
Msimamo TBC kutorusha ‘laivu’ uko palepale
By:
Unknown
On: 22:26
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa usitishwaji wa matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) utabaki palepale.
“Msimamo wa TBC ni msimamo wa Serikali,” amesema Majaliwa jana wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kufahamu kauli ya serikali juu ya TBC kusitisha matangazo kwani ni haki ya wananchi kikatiba.
Waziri Mkuu alisema suala hilo lilishatolewa ufafanuzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kilichofanywa na TBC ni kubadilisha ratiba. “Huo ni mpango wa ndani wa taasisi yenyewe kujiendesha, msimamo wa TBC ni msimamo wa serikali,” alieleza.
Juzi, Nape alitoa kauli ya serikali kuhusu TBC na kubainisha kuwa, kabla ya kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja TBC wakati huo Televisheni ya Taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya Bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama Bungeni Leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya Bunge kwa siku husika.
Alisema baada ya kuanza kwa kurushwa kwa matangazo hayo ya Bunge moja kwa moja mwaka 2005, TBC imekuwa ikilazimika kulipia gharama ya Sh bilioni 4.2 kwa mwaka ili kuwezesha urushwaji huo. Pia imekuwa ikigharimia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo ya biashara.
Akitetea hoja juzi usiku Nape alisema kinachofanyika sasa cha kurekodi na kisha kurusha baadaye matangazo ya Bunge, si jambo geni kwani uzoefu unaonesha kutoka mabunge mengine mengi Afrika na baadhi ya nchi zilizoendelea, hazirushi matangazo yao moja kwa moja.
“Kilichofanyika ni kubadilisha muda,” alisema na kusisitiza matangazo ya moja kwa moja yataendelea kurushwa tangu saa 3:00 asubuhi mpaka saa 5 isipokuwa kama kutakuwa na jambo kubwa na baada ya hapo, shughuli zitakazoendelea bungeni zitarekodiwa na kuoneshwa kwenye kipindi cha Leo katika Bunge.
Nape alisema uzoefu unaonesha mabunge mengine mengi hayafanyi utaratibu huu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja siku nzima kama ilivyokuwa ikifanyika nchini. Alitoa mfano wa mabunge hayo ni pamoja na ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Kwa mujibu wa Nape, Australia wanarusha matangazo ya bunge kwa muda wa saa nne kwa wiki; Canada wanarusha kupitia cable. Kwa upande wa Uingereza, Nape alisema wana kipindi kinaitwa Today in Parliament ambacho alisema kinaoneshwa kwa saa moja na wakati mwingine wanaonesha maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu.
Waziri Nape alisema uamuzi uliofikiwa, umetokana na TBC yenyewe ambao waliiandikia serikali barua wakieleza tatizo la gharama kubwa wanazoingia katika kurusha matangazo ya moja kwa moja. “Haya ndiyo mazingira tuliyofikia baada ya kushauriana na TBC. Huu ulikuwa uamuzi wa ndani,” alisema.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema msimamo wa Serikali wa usitishwaji wa matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) utabaki palepale.
“Msimamo wa TBC ni msimamo wa Serikali,” amesema Majaliwa jana wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Kiongozi wa Upinzani Bungeni ambaye ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kufahamu kauli ya serikali juu ya TBC kusitisha matangazo kwani ni haki ya wananchi kikatiba.
Waziri Mkuu alisema suala hilo lilishatolewa ufafanuzi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na kilichofanywa na TBC ni kubadilisha ratiba. “Huo ni mpango wa ndani wa taasisi yenyewe kujiendesha, msimamo wa TBC ni msimamo wa serikali,” alieleza.
Juzi, Nape alitoa kauli ya serikali kuhusu TBC na kubainisha kuwa, kabla ya kuanza kurusha matangazo ya moja kwa moja TBC wakati huo Televisheni ya Taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya Bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama Bungeni Leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya Bunge kwa siku husika.
Alisema baada ya kuanza kwa kurushwa kwa matangazo hayo ya Bunge moja kwa moja mwaka 2005, TBC imekuwa ikilazimika kulipia gharama ya Sh bilioni 4.2 kwa mwaka ili kuwezesha urushwaji huo. Pia imekuwa ikigharimia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo ya biashara.
Akitetea hoja juzi usiku Nape alisema kinachofanyika sasa cha kurekodi na kisha kurusha baadaye matangazo ya Bunge, si jambo geni kwani uzoefu unaonesha kutoka mabunge mengine mengi Afrika na baadhi ya nchi zilizoendelea, hazirushi matangazo yao moja kwa moja.
“Kilichofanyika ni kubadilisha muda,” alisema na kusisitiza matangazo ya moja kwa moja yataendelea kurushwa tangu saa 3:00 asubuhi mpaka saa 5 isipokuwa kama kutakuwa na jambo kubwa na baada ya hapo, shughuli zitakazoendelea bungeni zitarekodiwa na kuoneshwa kwenye kipindi cha Leo katika Bunge.
Nape alisema uzoefu unaonesha mabunge mengine mengi hayafanyi utaratibu huu wa kurusha matangazo ya moja kwa moja siku nzima kama ilivyokuwa ikifanyika nchini. Alitoa mfano wa mabunge hayo ni pamoja na ya nchi za Jumuiya ya Madola.
Kwa mujibu wa Nape, Australia wanarusha matangazo ya bunge kwa muda wa saa nne kwa wiki; Canada wanarusha kupitia cable. Kwa upande wa Uingereza, Nape alisema wana kipindi kinaitwa Today in Parliament ambacho alisema kinaoneshwa kwa saa moja na wakati mwingine wanaonesha maswali ya moja kwa moja kwa Waziri Mkuu.
Waziri Nape alisema uamuzi uliofikiwa, umetokana na TBC yenyewe ambao waliiandikia serikali barua wakieleza tatizo la gharama kubwa wanazoingia katika kurusha matangazo ya moja kwa moja. “Haya ndiyo mazingira tuliyofikia baada ya kushauriana na TBC. Huu ulikuwa uamuzi wa ndani,” alisema.
Chanzo Gazeti la HabariLeo.
Kivuko Kilombero chapinduka, watu kadhaa wafa
By:
Unknown
On: 22:20
Kivuko cha Mv Kilombero 11 mkoani Morogoro kikiwa kimezama kwenye mto Kilombero jana.
WATU kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya kivuko cha Mv Kilombero 11 kinachovusha watu na magari katika mto Kilombero mkoani Morogoro, kupinduka na kuzama. Ajali hiyo ilitokea wakati kikitokea wilaya ya Ulanga kwenda upande wa Ifakara wilaya ya Kilombero.
Kivuko hicho ambacho idadi ya abiria waliokuwemo hakijafahamika mara moja, kilibeba pia pikipiki, bajaji, baiskeli na magari kadhaa likiwemo la Benki ya CRDB Tawi la Ifakara, ambalo dereva wake anahofiwa kuzama.
Hata hivyo, akitoa taarifa ya serikali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alisema kivuko hicho kilikuwa na abiria 31, magari matatu na bajaji mbili.
Mhagama alisema abiria 30 walifanikiwa kuokolewa na maiti mmoja amepatikana. Aidha, Mkuu wa kivuko hicho, Fadhir Haroub alisema kilikuwa katika safari ya mwisho siku hiyo na kwamba kilipofika katikati ya mto, ulitokea upepo mkali na kukisukuma na nahodha alijitahidi kukiokoa, lakini ikashindikana na hatimaye kugonga nguzo za daraja la muda, kisha kusimama na kuzama.
Pamoja na hayo, alisema kilikuwa na magari matatu likiwemo lori aina ya Fuso lililobeba mchele na Land Cruiser mbili, moja ni ya benki ya CRDB na lingine la Kampuni ya Mitiki -KVTC na aina nyingine ya usafiri zikiwemo bajaj, bodaboda na baiskeli na vyote vimezama na kutojulikana kwa idadi ya watu waliofariki.
Katika ajali hiyo, watu wapatao 31 walijiokoa baada ya kuvaa ‘live jacket’ zinazohifadhiwa kama tahadhari ndani ya kivuko hicho, akiwemo Meneja wa CRDB Tawi la Ifakara, Joel Mwageni na wenzake wawili.
Hiyo ni ajali ya pili ya kuzama kwa kivuko katika mto Kilombero, ya kwanza ikiwa ni ya Mv Kiu kilichokuwa na kamba na kusukumwa na boti, kilichopinduka na kuzama majini mwaka 2002 na watu kupoteza maisha.
Baada ya hicho kuzama, serikali ilinunua kivuko kingine cha Mv Kilombero I ambacho kilizinduliwa Oktoba 12, 2002 kikiwa na uwezo wa kubeba tani 50 abiria na mizigo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Leonard Paulo, tukio la kupinduka na kuzama kwa kivuko hicho, lilitokea saa 1:15 juzi usiku kilipokuwa kinafanya safari kutokea upande wa Ulanga kuelekea upande wa Ifakara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika eneo la tukio, aliahidi kushirikiana na wananchi wa wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi katika uokozi kwa kutuma vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutafuta miili ya watu waliofariki dunia kwa ajali ya kuzama kivuko hicho.
Alisema serikali imeweka mkakati wa kuharakisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero na tayari mkandarasi, Kampuni ya M/S China Railway 15 Group Corporation amepatiwa Sh milioni 885 kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa, Dk Rajab Rutengwe, alikuwepo mjini Ifakara kwa ajili ya kupata taarifa sahihi na hatua za kuchukuliwa, zikiwemo za kibinadamu na urejeshaji wa huduma za usafiri kati ya Kilombero na Ulanga.
Chanzo Gazeti la habariLeo.
WATU kadhaa wanahofiwa kufa maji baada ya kivuko cha Mv Kilombero 11 kinachovusha watu na magari katika mto Kilombero mkoani Morogoro, kupinduka na kuzama. Ajali hiyo ilitokea wakati kikitokea wilaya ya Ulanga kwenda upande wa Ifakara wilaya ya Kilombero.
Kivuko hicho ambacho idadi ya abiria waliokuwemo hakijafahamika mara moja, kilibeba pia pikipiki, bajaji, baiskeli na magari kadhaa likiwemo la Benki ya CRDB Tawi la Ifakara, ambalo dereva wake anahofiwa kuzama.
Hata hivyo, akitoa taarifa ya serikali bungeni jana, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama alisema kivuko hicho kilikuwa na abiria 31, magari matatu na bajaji mbili.
Mhagama alisema abiria 30 walifanikiwa kuokolewa na maiti mmoja amepatikana. Aidha, Mkuu wa kivuko hicho, Fadhir Haroub alisema kilikuwa katika safari ya mwisho siku hiyo na kwamba kilipofika katikati ya mto, ulitokea upepo mkali na kukisukuma na nahodha alijitahidi kukiokoa, lakini ikashindikana na hatimaye kugonga nguzo za daraja la muda, kisha kusimama na kuzama.
Pamoja na hayo, alisema kilikuwa na magari matatu likiwemo lori aina ya Fuso lililobeba mchele na Land Cruiser mbili, moja ni ya benki ya CRDB na lingine la Kampuni ya Mitiki -KVTC na aina nyingine ya usafiri zikiwemo bajaj, bodaboda na baiskeli na vyote vimezama na kutojulikana kwa idadi ya watu waliofariki.
Katika ajali hiyo, watu wapatao 31 walijiokoa baada ya kuvaa ‘live jacket’ zinazohifadhiwa kama tahadhari ndani ya kivuko hicho, akiwemo Meneja wa CRDB Tawi la Ifakara, Joel Mwageni na wenzake wawili.
Hiyo ni ajali ya pili ya kuzama kwa kivuko katika mto Kilombero, ya kwanza ikiwa ni ya Mv Kiu kilichokuwa na kamba na kusukumwa na boti, kilichopinduka na kuzama majini mwaka 2002 na watu kupoteza maisha.
Baada ya hicho kuzama, serikali ilinunua kivuko kingine cha Mv Kilombero I ambacho kilizinduliwa Oktoba 12, 2002 kikiwa na uwezo wa kubeba tani 50 abiria na mizigo. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Leonard Paulo, tukio la kupinduka na kuzama kwa kivuko hicho, lilitokea saa 1:15 juzi usiku kilipokuwa kinafanya safari kutokea upande wa Ulanga kuelekea upande wa Ifakara.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiwa katika eneo la tukio, aliahidi kushirikiana na wananchi wa wilaya za Ulanga, Kilombero na Malinyi katika uokozi kwa kutuma vikosi vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kutafuta miili ya watu waliofariki dunia kwa ajali ya kuzama kivuko hicho.
Alisema serikali imeweka mkakati wa kuharakisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero na tayari mkandarasi, Kampuni ya M/S China Railway 15 Group Corporation amepatiwa Sh milioni 885 kukamilisha ujenzi huo.
Mkuu wa Mkoa, Dk Rajab Rutengwe, alikuwepo mjini Ifakara kwa ajili ya kupata taarifa sahihi na hatua za kuchukuliwa, zikiwemo za kibinadamu na urejeshaji wa huduma za usafiri kati ya Kilombero na Ulanga.
Chanzo Gazeti la habariLeo.
Makaburi matano yagunduliwa Bujumbura
By:
Unknown
On: 22:17
Shirika la
Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema
limeena picha za setilite zinazoonyesha mamia ya raia wa Burundi kuuawa
na baadae kuzikwa katika kaburi la watu wengi.
Amnesty limesema
sehemu za picha hizo zinaonyesha makaburi ya watu wengi yapatayo matano
katika eneo la Buringa viungani mwa mji mkuu wa Bujumbura.Shirika hilo linaongeza kuwa uchunguzi wao wa kitaalamu unafanana na ule ambao wameupata kutoka kwa mashahidi kuwa kuna makaburi mengine ya pamoja ya watu waliouwawa siku ya tarehe 11,desemba,siku ambayo ilishuhudia machafuko makubwa mjini Bujumbura.
Ripoti hiyo imekuja siku chache kabla ya mkutano wa viongozi wa umoja wa Afrika kukutana kujadili hatima ya mgogoro wa Burundi huko Ethiopia.
Mgogoro wa Burundi ulianza april mwaka uliopita, wakati ambapo raisi Pierre Nkurunzinza alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi kwa awamu ya tatu na kuchaguliwa tena kuwa raisi mwezi july mwaka wa jana.
Chanzo BBC Swahili.
Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni tena.......Ni Baada ya Naibu Spika Tulia Ackson Kuwanyima Muongozo ili Waongee
By:
Unknown
On: 22:12
Hali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge.
Hali
hiyo imetokea baada ya Naibu Spika Tulia Mwansasu kumtaka katibu wa
Bunge kuarifu bunge ratiba inayoendelea, ambapo katibu wa Bunge
alibainisha kwamba kazi ya ratiba ya leo inaonyesha kwamba ni kuchangia
hotuba ya Rais aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge.
Baada ya hapo wabunge wa upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu Spika, ambapo Naibu spika alimruhusu Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.
Mbunge huyo aliuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa wanafunzi kutozwa michango katika jimbo lake.
Naibu wa spika akitoa majibu ya muongozo huo alisema kwamba serikali inatambua matatizo yanayojitokeza na inayafanyia kazi
Jambo hilo liliwakasirisha wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika aliwakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea,hali ambayo iliwafanya wabunge wa upinzani wasuse na kutoka nje.
Baada ya hapo wabunge wa upinzani waliomba miongozo kutoka kwa Naibu Spika, ambapo Naibu spika alimruhusu Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko.
Mbunge huyo aliuliza swali kuhusu mapungufu yaliyojitokeza kwa elimu bure kwa wanafunzi kutozwa michango katika jimbo lake.
Naibu wa spika akitoa majibu ya muongozo huo alisema kwamba serikali inatambua matatizo yanayojitokeza na inayafanyia kazi
Jambo hilo liliwakasirisha wabunge wa upinzani na kuzidi kuomba miongozo ambapo Naibu Spika aliwakataza na kuruhusu ratiba iliyo mbele ya bunge kuendelea,hali ambayo iliwafanya wabunge wa upinzani wasuse na kutoka nje.
==>Wabunge wa CCM wanaendelea kujadili Hotuba ya Rais.
Credit;Mpekuzi blog
Wagombea wamkejeli Trump kwenye mdahalo
By:
Unknown
On: 22:10
Wagombea urais wa
chama cha Republican nchini Marekani wamemkejeli Donald Trump baada yake
kususia mdahalo wa kupeperushwa runingani katika jimbo la Iowa.
Aliamua
kusususia mdahalo huo wa shirika la Fox News baada ya shirika hilo
kukataa kumuondoa msimamizi wa mdahalo Megyn Kelly, ambaye Bw Trump
amemtuhumu kwa kuwa na mapendeleo.Mfanyabiashara huyo tajiri badala yake aliandaa hafla ya kuchangisha pesa, za kuwasaidia wanajeshi wastaafu.
Wapiga kura jimbo la Iowa watapiga kura Jumatatu kuchagua mgombea wao katika kila chama.
Lakini kutokuwepo kwa Trump katika mdahalo huo mjini Des Moines kulijitokeza wazi, na wagombea saba wanaoshindana naye walihisi kutokuwepo kwake.
Seneta wa Texas Ted Cruz aligusia hilo kwa ucheshi dakika za kwanza za mdahalo na kuwakejeli wapinzani wake.
"Mimi ni wazimu na kila mtu katika jukwaa hili ni mjinga, mnene na asiyevutia, na Ben [Carson], wewe ni daktari mbaya wa upasuaji,” alisema, huku akijaribu kumuiga Trump, ambaye hakuwepo.
Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush pia alimchokoza mfanyabiashara huyo tajiri kutoka New York, ambaye amekuwa akimshambulia Bw Bush midahalo ya awali.
- Trump alidhani mji wa Paris uko Ujerumani?
- Trump azungumzia video ya al-Shabab
- Trump amshukuru Putin kwa kumsifia
Mengine makuu yaliyojitokeza:
- Seneta wa Florida Marco Rubio alitetea msimamo wake wa awali wa kufunga misikiti ambayo inatumiwa kueneza itikadi kali
- Pia aliahidi kuvunja mkataba wa nyuklia na Iran siku ya kwanza akiwa rais.
- Seneta wa Texas Ted Cruz alisema: "Nitawawinda Isis [IS] popote walipo na kuwaangamiza "
- Gavana wa New Jersey Chris Christie alisema hajui lolote kuhusu misongamano ya magari ambayo inadaiwa kusababishwa makusudi na wasaidizi wake
- Gavana wa zamani wa Florida Jeb Bush amesema wanajeshi wa Marekani waliowahi kupigana vijani wanafaa kupata heshima zaidi kuliko wanavyopata sasa chini ya utawala wa Obama
- Seneta wa Kentucky Paul alieleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mchango wa Marekani kijeshi nchini Syria
“Unaponyanyaswa, lazima usimame na kutetea haki zako,” amesema, akirejelea mzozo wake na Fox News.
“Lazima tusimame kidete kama watu na kutetea taifa letu iwapo tunanyanyaswa.”
Wengi katika mitandao ya kijamii walionekana kukubali kwamba mdahalo huo wa Fox News ulimkosa sana Trump.
Lakini wengine walisema kukosekana kwake kulisaidia wagombea wengine, ambao hawajakuwa wakisikika kutokana na ‘ubabe’ wa Trump, kusikika.
Uchaguzi wa Iowa Jumatatu ijayo utakwua mtihani wa kwanza kamili kwa wagombea, na mwanzo tu wa msururu wa uchaguzi wa kuwachagua wajumbe wa vyama vya Republican na Democrats.
Kinyume na uchaguzi wa kawaida wa wagombea, ambapo kura za siri hupigwa, uchaguzi wa Iowa huwa ni mkutano wa wagombea wa vyama waliosajiliwa ambao kwanza huwajadili wagombea na kisha kupiga kura zao.
Chanzo BBC Swahili.
Breaking News: CUF Wagoma Kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar
By:
Unknown
On: 22:07
Azimio
La Baraza Kuu La Uongozi La Taifa Kuhusu Tangazo La Mwenyekiti Wa Tume
Ya Uchaguzi Ya Zanzibar La Kuitisha Uchaguzi Wa Marudio Zanzibar
Baraza
Kuu la Uongozi la Taifa la THE CIVIC UNITED FRONT (CUF – Chama Cha
Wananchi), likiwa ndiyo chombo cha juu cha maamuzi katika Chama baada ya
Mkutano Mkuu wa Taifa, limefanya kikao cha dharura leo, tarehe 28
Januari, 2016, katika Ofisi Kuu ya CUF, mjini Dar es Salaam.
Kikao
hicho kilikuwa na ajenda moja tu, ambayo ni kufanya maamuzi kuhusiana
na tangazo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar la kuitisha
uchaguzi wa marudio.
Baada
ya kujadili kwa kina tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya
Zanzibar, Jecha Salum Jecha, la kuitisha uchaguzi wa marudio tarehe 20
Machi, 2016 na mwenendo mzima wa hali ya kisiasa Zanzibar tokea alipotoa
tamko lake batili la tarehe 28 Oktoba, 2015 kudai kwamba amefuta
uchaguzi mkuu wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 na matokeo yake, Baraza Kuu la Uongozi la Taifa limefikia maazimio yafuatayo:
1.
KWAMBA Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umeshafanyika tarehe 25 Oktoba, 2015,
ambapo kwa upande wa uchaguzi wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na
Madiwani ulikwisha kamilika na washindi wote kupewa shahada za
kuwathibitisha na kuwatambua kama washindi halali.
Kwa
upande wa uchaguzi wa Rais wa Zanzibar, matokeo yalikwisha bandikwa nje
ya vituo vya majumuisho vya majimbo yote 54. Kilichokuwa kinaendelea
baada ya hapo ni kuhakiki matokeo hayo kutoka majimboni na kazi hiyo
ilikwishakamilika kwa majimbo 40 na katika hayo, matokeo ya uchaguzi wa
Rais kwa majimbo 31 yalikwishatangazwa kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi, Jecha Salum Jecha, kutangaza isivyo halali kwamba ameufuta
uchaguzi huo.
2. KWAMBA Chama Cha Wananchi (CUF) hakitoshiriki katika uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 kwa sababu uchaguzi huo si halali kwani uchaguzi halali ulishafanyika.
3.
KWAMBA linatoa wito kwa Wazanzibari wote wanaoipenda nchi yao na ambao
wanaamini katika utawala wa sheria, demokrasia na kuheshimu Katiba na
Sheria za nchi yetu kutoshiriki katika uchaguzi huo usio halali wa marudio.
4.
KWAMBA sababu kuu ya Baraza Kuu kufikia maamuzi haya ni kutokana na
matamko yote mawili ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha
Salum Jecha, kutokuwa halali na kwenda kinyume na Katiba ya Zanzibar na
Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.
Hakuna
kifungu chochote cha Katiba ya Zanzibar au Sheria ya Uchaguzi ya
Zanzibar kinachotoa uwezo kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar
na hata kwa Tume yenyewe kufuta uchaguzi au kuitisha uchaguzi wa
marudio.
5.
KWAMBA linazipongeza na limetiwa moyo sana na taasisi na jumuiya zote
za kimataifa na kikanda zikiwa ni pamoja na Jumuiya ya Madola (The
Commonwealth), Umoja wa Ulaya (European Union), Umoja wa Afrika (African
Union), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na nchi za Marekani na
Uingereza kwa msimamo wao wa kuungana na Wazanzibari na kutetea haki yao
ya kidemokrasia na maamuzi halali waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na kutaka mchakato wa uchaguzi huo ukamilishwe
na matokeo yake kutangazwa.
6.
KWAMBA linazipongeza na kutiwa moyo pia na taasisi za hapa nchini
zikiwemo taasisi na jumuiya za kidini, taasisi za haki za binadamu,
vyombo huru vya habari, vyama vyengine vya siasa na Wazanzibari na
Watanzania wote wanaopenda amani na demokrasia kwa msimamo wao wa
kutetea maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya katika uchaguzi mkuu wa
tarehe 25 Oktoba, 2015 na kuendelea kusisitiza haja ya kuheshimu na
kufuata Katiba na Sheria za nchi yetu na pia haja na umuhimu wa kutunza
amani ya nchi yetu kwa kutaka haki itendeke.
Baraza
Kuu linazihakikishia taasisi na jumuiya hizo zote na pia kuwahakikishia
Wazanzibari na Watanzania wote kwamba CUF itaendelea kusimama kidete
katika kulinda na kutetea Katiba na Sheria za nchi yetu na pia kutetea
maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.
7.
KWAMBA limesikitishwa na kushangazwa na kitendo cha Msajili wa Vyama
vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, kuandika barua na kutoa taarifa kwa
vyombo vya habari kutaka vyama vya siasa vishiriki uchaguzi wa marudio
uliopangwa kufanyika tarehe 20 Machi, 2016 bila ya kujali kwamba
uchaguzi huo ni haramu na unakiuka matakwa ya Katiba ya Zanzibar na
Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar Nam. 11 ya 1984.
Baraza
Kuu halikutarajia mtu mwenye hadhi ya Ujaji kufanya kazi ya kutumikia
maslahi ya watawala ambao wameamua kuvunja Katiba na Sheria za nchi yetu
na kukanyanga misingi ya haki na demokrasia huku akishindwa kukemea
uhuni mkubwa uliofanywa wa kubaka demokrasia na haki za watu.
8.
KWAMBA limesikitishwa na kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dk. John Pombe Magufuli, kukwepa dhamana na wajibu
wake kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu kwa kuiacha njiani kazi
aliyoianza ya kutafuta ufumbuzi wa mkwamo wa uchaguzi Zanzibar.
Baraza
Kuu linamtaka Rais Magufuli kujitathmini na kujiuliza anajiweka vipi na
kutoa taswira gani mbele ya macho ya Watanzania na jumuiya ya kimataifa
kutokana na kutosimamia ahadi yake aliyoitoa mbele ya Watanzania wakati
akilizindua Bunge jipya kwamba atafanya kazi na vyama vya CUF na CCM
ili kuupatia ufumbuzi mkwamo huu.
9.
KWAMBA linalaani matumizi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na
usalama vya Jamhuri ya Muungano na Vikosi vya SMZ dhidi ya wananchi
wasio na hatia na ambao wamekuwa watulivu licha ya vitendo vingi vya
uchokozi wa makusudi na hata mashambulizi ya hujuma dhidi yao
yanayofanywa na makundi ya vijana wa CCM waliowekwa katika makambi
kadhaa kisiwani Unguja.
10.
KWAMBA linaitaka jumuiya ya kimataifa na hasa taasisi zinazosimamia
haki za binadamu na zinazopambana na makosa ya jinai kimataifa ikiwemo
Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
(International Criminal Court – ICC) kufanya uchunguzi wa kauli na
matendo ya uhalifu, uvunjwaji mkubwa wa haki za binadamu na ubaguzi
ambao umekuwa ukifanywa dhidi ya wananchi wa Zanzibar na kuchukua hatua
dhidi ya watu walio nyuma ya maamuzi na utekelezaji wa matukio hayo.
11.
KWAMBA linawapongeza wananchi wa Zanzibar kwa kuonesha ukomavu wa hali
ya juu na kuwa watulivu licha ya machungu makubwa waliyoyapitia na
wanayoendelea kuyapitia tokea pale maamuzi yao yalipopinduliwa na CCM
kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum
Jecha.
Baraza
Kuu linatoa wito kwa Wazanzibari wote kuungana pamoja chini ya chama
chao cha CUF walichokipa ridhaa halali kupitia uchaguzi mkuu wa tarehe
25 Oktoba, 2015 kutetea maamuzi yao waliyoyafanya kupitia sanduku la
kura kwa njia za amani.
Baraza
Kuu linawasisitiza tena Wazanzibari kwamba waendelee kutunza amani ya
nchi yetu na kutambua kwamba kutunza amani si udhaifu bali ni jambo
linaloipa nguvu jumuiya ya kimataifa kufuatilia haki za kidemokrasia za
wananchi wa Zanzibar.
12.
Baraza Kuu la Uongozi la Taifa linawatahadharisha CCM na watawala
wasiowajali na kuwaheshimu wananchi kwamba zama za utawala wa mabavu
usioheshimu Katiba na Sheria za nchi hazina nafasi tena katika dunia ya
leo. Baraza Kuu lina imani kwamba HAKI ITASHINDA.
LIMETOLEWA NA:
BARAZA KUU LA UONGOZI LA TAIFA
THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF – Chama Cha Wananchi)
DAR ES SALAAM
28 JANUARI, 2016
Credit;Mpekuzi blog
Subscribe to:
Posts (Atom)