Nchi za Urusi,Misri na Senegal
zimepinga mapendekezo ya adhabu ya kurejeshwa nyumbani kwa kikosi kizima
cha kulinda amani iwapo itabainika askari kufanya ukatili wa kingono.
Badala yake wametaka adhabu hiyo kuwalenga askari watakaobainika tu.
Umoja
wa mataifa umetoa mapendekezo hayo kwa lengo la kutokomeza unyanyasaji
wa kijinsia unaofanywa na baadhi ya walinzi wa vikosi vya kulinda amani
amani dhidi ya watoto.Mapendekezo hayo yanaungwa mkono na katibu mkuu wa umoja wa mataifa,Ban Ki-Moon ambaye ameliambia baraza la usalama kutilia mkazo jambo hilo.
Adhabu hiyo imetajwa kuwa itatakiwa kumlenga mhusika tu na si kikosi chote.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment