Katibu
mkuu mpya wa Chadema atajulikana leo wakati Mwenyekiti wa chama hicho,
Freeman Mbowe atakapowasilisha jina la mtu anayempendekeza kushika
wadhifa huo.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalim alisema jana kuwa jina hilo
linatarajiwa kuwasilishwa mbele ya kikao cha Baraza Kuu kinachoanza
jijini Mwanza leo.
"Moshi
mweupe kuhusu jina la katibu mkuu mpya utaonekana Jumamosi mchana
(leo). Mimi na Naibu Katibu Mkuu mwenzangu John Mnyika tuko tayari
kumpokea bosi mpya,” alisema Mwalimu.
Katika
kikoa chake na waandishi wa habari kilichohudhuriwa na Mnyika, Kaimu
Katibu Mkuu huyo alisema hadi sasa, hakuna yeyote miongoni mwa viongozi
na wanachama wa Chadema anayejua kwa hakika nani atarithi mikoba hiyo
iliyoachwa na Dk Willibrod Slaa zaidi ya Mbowe.
Alipoulizwa
jana, Mbowe hakutaka kuzungumzia suala hilo kwa undani zaidi ya kuahidi
kumteua katibu mkuu atakayemudu kubeba dhamana ya kuivusha Chadema
salama katika harakati za kushika dola katika uchaguzi mkuu ujao wa
mwaka 2020.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Profesa Mwesiga Baregu alisema: “Tunaweza
kufikia uamuzi kwa maridhiano bila hata wajumbe kulazimika kupiga kura.
Hilo naweza kukuhakikishia kwa sababu mimi ndiye mwenyekiti wa kamati
ya maridhiano.”
Pamoja
na kupitisha jina la katibu mkuu, vikao vikuu vya Chadema ambavyo kwa
mara ya kwanza vimefanyika nje ya Dar es Salaam, pia vinatarajiwa
kujadili na kuamua mpango mkakati wa kisiasa wa miaka mitano kuanzia
sasa hadi 2021, kupitisha bajeti ya chama kwa kipindi hicho na kufanya
marekebisho ya katiba, kanuni na miongozo ya mabaraza.
Credit;Mpekuzi blog
0 comments:
Post a Comment