Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameagiza kufanyika kwa uchunguzi
jengo la Machinga Complex kubaini uhalali wa mkataba uliowezesha ujenzi
wa jengo hilo, ikiwa ni pamoja na gharama halisi za ujenzi.
Alisema
hayo kutokana na jengo hilo kuwa na deni la zaidi ya Sh bilioni 36,
kiasi ambacho ni mara tatu ya thamani halisi ya jengo hilo na kuleta
shaka ya ufisadi ndani yake. Jengo hilo lina thamani ya Sh bilioni 12.
Alisema
kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa itaanza kufanya uchambuzi wa
mkataba ili kupata uhalali wa gharama na kujua kiwango kinachostahili
kulipwa na wafanyabiashara hao.
“Katika
miradi mingi duniani huu ni wa aina yake, mradi ambao kabla haujaanza
unaweka jiwe la msingi unaanza kudaiwa benki, mpaka unakuja kumaliza
deni lako ni kubwa linakaribia robo mbili au tatu ya mkopo wenyewe,
kabla hata hujaanza kupangisha hata mtu.
“Kwa
takwimu zinaonesha tumekopeshwa na jengo limejengwa Sh bilioni 12.7,
lakini mpaka dakika hii mnadaiwa Sh bilioni 36 na nyinyi ndio mnatakiwa
kuzilipa, sasa kwa maelezo hayo ndio mnapata picha kwa nini tumeamua
kujipa muda,” alisema Makonda.
Alisema
katika maelezo ya awali yanaonesha kuwa jengo hilo lina mkanganyiko
mkubwa na inawezekana kuwa ni miongoni mwa miradi iliyofanyiwa ufisadi
mkubwa.
Hivi
karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, George Simbachawene
aliifuta bodi inayosimamia jengo hilo na kumsimamisha kazi meneja
anayesimamia jengo hilo na kumtaka kwenda katika ofisi za jiji kwa ajili
ya kumpangia kazi nyingine.
Katika
hatua nyingine, Simbachawene alilikabidhi jengo hilo kwa Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuwaingiza
wafanyabiashara bila masharti huku ukiangaliwa utaratibu mpya kwa
wafanyabiashara hao.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment