Wagombea urais
waliosalia katika chama cha Democratic, Hillary Clinton na Bernie
Sanders, wamejibizana vikali katika mdahalo uliofanyika katika jiji la
New York.
Kila mmoja ametilia shaka uwezo wa mpinzani wake kufanya
uamuzi wa busara kuhusu masuala kama vile kudhibiti benki Wall Street,
kudhibiti umiliki wa silaha na ujira wa chini.Jimbo la New York litafanya mchujo wake Jumanne.
Bw Sanders amemkosoa Bi Clinton kwa kuunga mkono vita vya Iraq na kutetea mikataba ya biashara huru.
Lakini naye Bi Clinton amemtuhumu Bw Sanders na kusema hawezi kutekeleza hata sera zake mwenyewe, mfano kuvunja udhibiti wa benki kuu za Wall Street.
Wote wawili wana uhusiano mkubwa na jimbo hilo la New York.
Bw Sanders alizaliwa huko naye Bi Clinton amekuwa seneta wa jimbo hilo kwa miaka minane.
Mdahalo huo wa runingani umefanyika eneo la Brooklyn.
Bw Sanders ameshinda majimbo saba kati ya manane yaliyofanya mchujo karibuni jambo lililomuwezesha kupunguza uongozi wa Bi Clinton katika mchujo wa chama hicho.
Bi Clinton hata hivyo bado anajivunia uongozi mkubwa.
Uchaguzi mkuu nchini Marekani utafanyika mwezi Novemba.
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment