Monday, 18 April 2016

Tagged Under:

NEEC Yaja na Ajira Yangu Kuwainua vijana Kiuchumi

By: Unknown On: 21:16
  • Share The Gag

  • Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanzisha mpango wa Ajira Yangu wenye lengo la kuwainua vijana kiuchumi vijana.

    Akizungumza jana, Katibu wa Baraza hilo, Beng’i Issa alisema mpango huo unafanyika kwa mfumo wa shindano kwa kuwashindanisha vijana nchi nzima kuanzia miaka 18 hadi 35.

    “Mpango huu umebuniwa kwa ajili ya vijana kupata ujuzi wa kuanzisha na kuendeleza biashara na kuwawezesha mitaji, ili waweze kuanza au kuboresha biashara zao, na kutengeneza nafasi za ajira kwao wenyewe na kwa vijana wengine pia,” alisema Issa .

    Issa alisema Ajira Yangu Business Plan Competition itahusisha vijana wanaotaka kuanza biashara au wanaotaka kupanua na kuboresha biashara zao bila kujali kiwango cha elimu.

    Alisema vijana hao wanatakiwa kuja na mipango rasmi ya biashara kwa ajili ya mashindano katika sekta za kilimo na kilimo usindikaji, ikiwa ni pamoja na viwanda, vyombo vya habari, masoko na mawasiliano, michezo, vifaa, sanaa na utamaduni, utalii na burudani.

    Alisema mipango hiyo pia ilenge katika mazingira na utunzaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na biashara ya kijamii, biashara inayohusu habari na mawasiliano, teknolojia, ikiwa ni pamoja na usindikaji biashara.

    Alisema awamu ya kwanza ya mpango huo itawahusu vijana kujaza fomu ya ushiriki zilizo kwenye tovuti za ILO na NEEC ambapo mwisho wa maombi utakuwa Mei 9 mwaka huu kuanzia jana.

    Issa alisema awamu ya pili itahusisha mafunzo ya siku moja ya kina ya mipango ya biashara ambayo itawakutanisha vijana 25 watakaochaguliwa na baadaye vijana hao watawasilisha mipango yao kwa majaji na wawekezaji na hapo vijana 10 watapewa mitaji yenye jumla ya dola za Marekani 75,000 (zaidi ya Sh milioni 150) .

    Mratibu Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO), Dk Annamaria Kiaga, alitaka vijana wengi kujitokeza kwani shirika lake lina mipango ya baadaye ya kuinua vijana.
    Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga katikati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam
    Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) jijini Daar es Salaam jana  kuhusiana na Progrmu ya umoja wa mataifa kuhusu Ajira kwa vijana. Kushoto ni Mratibu Mtendaji wa Mradi wa Maendeleo wa umoja wa Mtaifa,Anamarie Kiaga.
    ==

    Credit; Mpekuzi Blog 

    0 comments:

    Post a Comment