Mwenyekiti
wa Kijiji cha Munge kilichopo kata ya Donyomurwa, wilaya ya Siha mkoani
Kilimanjaro, Peter Laiza, ameswekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya
hiyo, Dk Charles Mlingwa, kutokana na kuwafukuza Maofisa Ardhi waliokuwa
katika mpango wa kutatua mgogoro wa ardhi.
Mgogoro
huo wa ardhi unadaiwa kukihusu kijiji cha Munge kinachoongozwa na
Mwenyekiti huyo pamoja na eneo la Kilelepori linalotumiwa na Chuo cha
Taaluma ya Polisi (MPA).
Katika
kuupatia ufumbuzi mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya aliwatuma Maofisa Ardhi
ili upimaji ufanyike katika baadhi ya maeneo ya wananchi.
Hata
hivyo, inadaiwa kwamba Dk Mlingwa alichukua hatua hiyo bila kutoa
taarifa kwa uongozi wa kijiji, hali iliyomlazimu mwenyekiti huyo
kuwakataza maofisa hao kufanya kazi hiyo kijijini kwake.
Kamanda
wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa, alithibitisha
kukamatwa na kuwekwa ndani kwa mwenyekiti huyo, kwa kile alichoeleza ni
kutokana na amri ya Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk Mlingwa.
Hata
hivyo, Diwani wa Kata ya Donyomurwa, Luite Ndoss, alisema hakuwa na
taarifa zozote za kushikiliwa kwa kiongozi huyo, bali taarifa hizo
alizipata baada ya kufika katika kituo cha Polisi akiwa anafuatilia
mambo yake binafsi.
Kutokana
na mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya aliitisha kikao cha Serikali ya Kijiji
Machi 30 lakini mwenyekiti huyo hakuweza kuhudhuria kwa sababu shauri la
mgogoro huo liko katika Mahakama ya Ardhi. Diwani Ndoss pia
hakuhudhuria kikao hicho.
“Kitendo
cha Mkuu wa Wilaya kutoa amri ya Mwenyekiti wa Kijiji cha Munge kuwekwa
ndani ni jambo la uonevu, na kitendo hicho kinazidi kuongeza mgogoro
kati ya wananchi na Mkuu wa Wilaya,” alidai Ndoss.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment