Daladala
zinazofanya safari zake katikati ya jiji la Dar es Salaam zimetakiwa
kuondoka ifikapo Mei 2 Mwaka huu ilikupisha mradi wa mabasi yaendayo
kasi kuweza kufanya shughuli zake kuanzia hiyo Mei 10.
Juzi,
Waziri wa Nchi, ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), George Simbachawene alisema mradi huo utaanza kutoa huduma
kwa wakazi wa jiji hilo Mei 10.
Msemaji
wa mradi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi
Mkoa wa Dar es Salaam (Dacoboa), Sabri Mabrouk alisema wamiliki wote wa
daladala walilipwa fidia ya kubadili njia.
“Wamiliki
wa mabasi walishalipwa fedha zao tangu Desemba mwaka jana, hakuna
anayedai na tumewapa siku saba kuondoka barabarani kabla ya Mei 10,’’ alisema.
Mabasi
hayo zaidi ya 30 ya Darts yalianza kupita kwenye njia zote za mradi
huo. Changamoto kubwa inayolalamikiwa ni muingiliano wa daladala, magari
binafsi, pikipiki na raia kupita bila tahadhari kwenye njia za mradi.
Moja ya mabasi hayo jana lilipata ajali baada ya kukwaruzana na pikipiki eneo la Kinondoni.
“Nasikitika
pikipiki zinapita wala madereva hawaangalii, wameshakwaruzana na basi
la mradi, sijui itakuwaje mradi utakapoanza, elimu inahitaji kwa
wananchi bila hivyo tutawapoteza wengi,” alisema Mabrouk
Alisema wamelazimika kufanya majaribio bila ya kubeba abiria kwa zaidi ya wiki kwa kuwa nauli mwafaka haijajulikana.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment