Thursday, 14 April 2016

Tagged Under:

Utafiti: Vijana wengi Tanzania ‘hawalitumikii taifa''

By: Unknown On: 22:53
  • Share The Gag
  • Utafiti huo uliangazia mwaka 2014/2015
    Utafiti umebaini kwamba asilimia 71 ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 wanatumia muda wao mwingi kwenye shughuli zisizo za uzalishaji mali.
    Badala yake hutumia muda huo kujihudumia kwenye gesti, baa, kulala na katika shughuli za starehe.
    Serikali imesema hali hii inaichelewesha Tanzania kuingia katika kundi la mataifa yenye uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.
    Bi Ruth Minja, ambaye ni mtakwimu mkuu katika ofisi ya taifa ya takwimu Tanzania, ndiye aliyeongoza utafiti huo wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa mwaka 2014/2015.
    Ripoti ya uchunguzi huo imezinduliwa leo Dar es Salaam Anasema waligundua kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa milioni 25 kutokana na kiashiria cha saa za kufanya kazi kupungua na baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa kazi kutokana na utendaji dhaifu.
    Ally Msaki, aliyemuwakilisha katibu mkuu katika ofisi ya waziri mkuu anayeshughulikia masuala ya kazi,vijana ajira na watu wenye ulemavu amewaangazia Watanzania walioko kwenye ajira, ambao wanapata kipato ambacho hakitoshelezi kuweza kumudu gharama za maisha.
    Amesema nafasi kama hizo za kazi hazina viwango vya ubora na ni kinyume cha maelekezo ya shirika la wafanya kazi duniani ILO.
    Ingawa Sera ya taifa ya ajira kwa Taifa la Tanzania kwa mwaka 2008 ilijikita zaidi katika kuongeza fursa za ajira na kufanikiwa katika lengo lake, kuna kasoro kwenye kipengele cha ubora wa ajira.
    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment