Friday, 22 April 2016

Tagged Under:

Siwema wa Nay wa Mitego Ahukumiwa Jela Miaka Miwili

By: Unknown On: 22:50
  • Share The Gag

  • Sheria  ya Makosa ya Mtandao ya Mwaka 2015 imemkumba mwanadada ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa staa wa Bongo fleva, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, Siwema anayeishi Mwanza baada ya kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka miwili.

    Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama Kuu ya Mkoani Mwanza ambapo Siwema amehukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kumtukuna matusi mtu kwa njia ya mtandao kitu ambacho ni kinyume cha sheria nchi. Siwema alituhumiwa kumtukana matusi kwa njia ya mtandao mlalamikaji ambaye anafahamika kwa jina la Deo.

    Akihojiwa na baadhi vyombo vya habari, mzazi mwenzake na Siwema ambaye ni Nay wa Mitego alikiri kupokea taarifa hizo za mzazi mwenziye kufungwa huku akisisitiza kuwa anaangalia uwezekano wa kumsaidia mwanamke huyo.

    “Taarifa nimezipokea ni kweli Mzazi mwenzangu (Siwema) amefungwa na ninakumbuka nilipoamka tu nikakutana na missed calls za ndugu zake kadhaa ambao wananifahamu nikahisi kuna kitu maana sio kawaida watu kunipigia mara kwa mara, kumpigia akaniambia Siwema amehukumiwa miaka miwili jela sikuamini ikanibidi nimpigie tena ndugu wa karibu naye akanithitibishia hivyo.

    “Kosa unajua mimi nilishasahau kwamba kitu chochote kichotokea kipindi cha nyuma kwasababu ni muda kidogo na pia sikuwa naye kwenye mawasiliano ila niliachoambiwa kuwa amehukumiwa miaka miwili kutoka na kosa lake, nimejikuta nimekuwa mnyonge nimeingia imani kusikia habari hiyo.

    “Napambana jinsi ninavyoweza kuona namna ninayoweza kumpa msaada kwa njia yoyote ili asiwe kwenye mazingira ambayo tayari ameshawekwa.” alisema Nay.

    Nay wa Mitego aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na kwa muda mrefu na Siwema na kubahatika kuzaa naye mtoto aitwaye Curtis ambapo baadaye walifarakana hivyo Nay akaamua kumchukua mtoto kutoka mikononi mwa mama yake japo ilimletea shida mpaka akalazimika kwenda kupima DNA na Curtis.
    Credit; Mpekuzi Blog 

    0 comments:

    Post a Comment