Wednesday, 6 April 2016

Tagged Under:

Bensouda: Kenya haikushirikiana na ICC

By: Unknown On: 22:14
  • Share The Gag
  • Kiongozi wa mashtaka wa ICC bi Fatou Bensouda
    Kiongozi wa mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu na makosa ya jinai ICC yenye makao yake makuu nchini Uholanzi, bi Fatou Bensouda ameilaumu serikali ya Kenya kwa kuhujumu kesi dhidi ya watuhumiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 naibu rais William Ruto na mwandishi Joshua arap Sang.
    Katika ujumbe wa video uliochapishwa kwenye mtandao wa Youtube bi Bensouda anasema kuwa mashdi wake walihongwa wengine wakatengwa baada ya kutishwa na kushinikizwa kujiondoa kama mashahidi.
    ''Tunasikita kuwa kutokana na shinikizo na hujuma dhidi ya mashahidi wetu kutoka kwa watu wenye uwezo mkubwa nchini Kenya, jopo la majaji wa mahakama ya kimataifa ya ICC lilishindwa kutoa hukumu kutokana na ushahidi halisi tulioyokuwa nayo.
    Katika tukio hili, mashahidi 17 wa upande wa mashtaka waliokuwa wameahidi kutoa ushahidi dhidi ya watuhumiwa walijiondoa wakihofia maisha yao.
    Naibu rais wa Kenya William Ruto Yamkini walikuwa wanatishiwa maisha yao, wengine walitengwa na jamii
    Licha ya serikali ya Kenya kuahidi kuwa ingeshirikiana na mahakama ya kimataifa ya ICC ukweli ni kwamba serikali ya Kenya haikutoa 100% ya ushirikiano na mahakama ya ICC.
    Hii ilisababisha afisi ya kiongozi wa mashtaka kukosa ushahidi uliohitajika kuthibitisha tuhuma dhidi ya washukiwa wakuu.
    Vizuizi tulivyowekewa na washirika wa watuhumiwa wakuu wa mauaji na makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotokea punde baada ya uchaguzi wa mwaka wa 2007 ulisababisha tukashindwa kuwawajibisha wale waliosababisha ghasia hizo na hivyo tumeshindwa kuwapa haki wale wahanga wa ghasia hizo.'' Taarifa hiyo ya kiongozi wa mashtaka ilisema.
    Bi Fatou Bensouda hata hivyo hakufa moyo anaiitaka serikali ya Kenya ichukue hatua kwa niaba ya wahanga wa machafuko hayo ya mwaka wa 2007 na kuwakamata mwandishi wa habari Walter Barasa, wakili Paul Gicheru na Philip Bett na kuwakabidhi kwa maafisa wa mahakama hiyo ya Uholanzi.
    Watatu hao wanatafutwa na mahakama hiyo ya ICC kwa madai ya kutoa hongo kwa mashahidi na kwa kuwatishia mashahidi wa ICC hadi wakajiondoa.
    Tayari vibali vya kukamatwa kwao vimeshatolewa.
    Hapo jana jopo la majaji Olga Herrera Carbuccia, Chile Eboe-Osuji na Robert Fremr lilikubaliana na bi Bensouda kuwa mashahidi wengi walihongwa na kutishiwa maisha hadi wakajiondoa kufuatia shinikizo kubwa la kisiasa na hivyo wakawaondolea mashtaka naibu wa rais William Ruto na mwandishi habari Joshua arap Sang .

    Chanzo BBC Swahili.

    0 comments:

    Post a Comment