Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress.
SERIKALI ya Marekani imesema itaendelea kutoa misaada katika sekta ya
afya na elimu nchini, ikiwa ni mwendelezo wa kuimarisha ushirikiano
wake na Tanzania.
Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress alisema hayo jana jijini
Dar es Salaam alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki,
Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga.
Childress akiwa ameongozana na viongozi wengine waandamizi wa ubalozi
wa Marekani, walikutana na Mahiga kuzungumzia mambo mbalimbali ya
ushirikiano wa nchi yao na Tanzania.
Alisema, Marekani itaendelea kutoa misaada yake kwa Tanzania na
hususan kwenye sekta ya afya na elimu, lengo likiwa kuimarisha sekta
hizo ili wananchi waweze kufanya kazi za uzalishaji na kuinua uchumi.
Aidha, katika mazungumzo hayo, walijadili jinsi ya kuimarisha masuala
ya kidiplomasia na namna ya kuzidisa usalama wa kikanda, kuinua uchumi
na kuhakikisha uhusiano baina ya mataifa hayo kwa manufaa ya nchi zao.
Chanzo HabariLeo.
Wednesday, 13 April 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment