Kampuni ya magari
ya Volkswagen imetangaza kuyanunua magari ya kampuni yake kutoka kwa
wateja nchini Marekani yapatayo nusu milioni kama sehemu ya kutimiza
makubaliano yaliyofikiwa na idara ya sheria ya Marekani dhidi ya
makampuni ya kutengeneza na kashfa ya uchafuzi wa hali ya hewa.
Jaji
kutoka San Francisco hajabainisha wazi kiasi ambacho wamiliki wa magari
hayo watalipwa na kampuni ya Volkswagen pale watakapo iuzia kampuni
hiyo magari yake wanayoyamiliki.Makubaliano mengine yaliyofikiwa ni kwamba Volkswagen itatakiwa kutoa fungu la fedha ili kuhamasisha tekinolojia ya kijani.
Wakili anayeiwakilisha kampuni ya Volkswagen Robert Giuffra,amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya jitihada zote kuhakikisha inapunguza uchafuzi wa hewa
Upande wa mashtaka ukiongozwa na wakili David Boies umesema unataraji haki itatendeka kwa wamiliki wa magari hayo.Joyce Ertel Hulbert,ni mmoja wa wamiliki wa magari aina ya Volkswagen yeye anadai anadai kampuni hiyo imemuangusha
.
Msemaji wa kampuni hiyo anasema wameonyesha ushirikiano wa kutosha katika kuchunguzwa kwao
Chanzo BBC Swahili.
0 comments:
Post a Comment