SerikaliI ya Korea imepanga kuleta nchini walimu wa masomo ya hisabati na sayansi kwa shule za sekondari, kusaidia kupunguza uhaba wa walimu wa masomo hayo.
Itatekeleza azma hiyo kupitia Mpango wake wa Kusambaza Walimu wa Kikorea katika nchi Zinazoendelea (KTDP).
Akizungumza
jana alipotembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais wa Taasisi ya
Elimu ya Kimataifa (NIIED), Kim Kwangho, alisema nchi yake imekuwa
ikisambaza walimu.
Alisema mpaka sasa wamesambaza walimu 61 katika nchi mbalimbali zinazoendelea; na mwaka huu watasambaza walimu 140 kwa nchi 15.
Alisema mpaka sasa wamesambaza walimu 61 katika nchi mbalimbali zinazoendelea; na mwaka huu watasambaza walimu 140 kwa nchi 15.
“Tumeona
katika kuunga mkono juhudi za serikali kuongeza walimu wa masomo ya
sayansi na kwa mara ya kwanza mwaka huu taasisi yetu itasambaza walimu
10 hapa Tanzania kati yao watano watahusika katika masomo ya hisabati na
wengine watano watahusika na masomo ya Sayansi,” alisema Kwang-ho.
Aidha
alisema licha ya kusambaza walimu hao, Serikali ya Korea inatoa
ufadhili kwa wanafunzi wenye vipaji kimataifa ili kuendeleza masomo yao
katika taasisi za elimu ya juu nchini kwao, lengo likiwa ni kusaidia
kukuza viongozi wa baadae wenye elimu.
Kwang-ho
alisema waombaji wa ufadhili huo ni wale waliosoma tu Shahada ya kwanza
na shahada ya Uzamili nchini; na haitawahusu wale wote ambao wamewahi
kusoma Korea.
Katika
hatua nyingine, Kwang-ho alisema Korea ina mpango wa kufungua kituo cha
kutoa kozi ya lugha ya Kikorea katika chuo kikuu hapa nchini, lengo
likiwa ni kupanua wigo wa fursa kwa wanafunzi wa Kitanzania kujifunza
lugha hiyo.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Masuala ya Mahusiano Kimataifa,
Opportuna Kweka alisema tayari rais huyo ameshakutana na Makamu Mkuu wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala na kujadili
uwezekano wa kuanzisha kituo hicho.
Credit; Mpekuzi Blog
0 comments:
Post a Comment